Mulamwah afichua ujanja na siri ya kufanikiwa kujenga jumba la kifahari kijijini

Mchekeshaji huyo alifichua kwamba amekuwa akiishi kwa nyumba ya kodi ya shii ngi elfu 9 kwa miaka kadhaa, kwani alikuwa na lengo la kufanikisha ndoto yake ya kujenga kijijini kwanza.

Muhtasari

• Alitamba na kusema kwamba nyumba mpya ambayo amehamia na mchumba wake Ruth K kodi ni shilingi elfu 70 kwa mwezi.

• Walihama siku chache baada ya kufanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza na Ruth K mapema mwezi jana.

Mulamwah na jumba lake la kifahari
Mulamwah na jumba lake la kifahari
Image: Facebook

Mchekeshaji Mulamwah ameonyesha maendeleo ya jumba lake la kifahari ambalo limekuwa chini ya ujenzi kwa takribani miaka miwili sasa.

Akionesha maendeleo hayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, mchekeshaji huyo ambaye pia ni mtangazaji kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini alifichua kwamba alipoanza, wengi hawakuamini kwamba angeumaliza mjengo wake.

Alionyesha picha ya mjengo ambao kwa asilimia kubwa unaelekea kukamilika na kusema kwamba amefanikisha ndoto hiyo licha ya wengi kuhisi kwamba asingeweza, mapema mwaka 2022 alipoanza mradi huo wa ujenzi.

Alitumia fursa hiyo kuwaasa mashabiki wake kwamba wasiwahi vutwa nyuma na maneno ya watu pindi wanapoamua kuanza kutekeleza jambo lao.

Pia alifichua siri ya kufanikiwa kujenga moja ya jumba la kifahari akisema kwamba siri ni kujifanya mjinga pindi watu wanapoibuka na maoni yao tofauti tofauti kuhusu maamuzi ya mradi wako.

“Mtu asiwahi kuambia huwezi … songa pole pole ila kwa usahihi. songa na kasi yako. Ujanja ni kujifanya fala tu,” alisema.

Hivi majuzi, Mulamwah alipokuwa akihama katika nyumba ya kupangisha ya chumba kimoja hadi nyumba ya vyumba vitatu, alisema kwamba sasa amepata nafasi ya kupumua angalau kidogo kwani nyumba yake ya kijijini Kitale pahali imefika inaelekea kukamilika kwa ujenzi.

Mchekeshaji huyo alifichua kwamba amekuwa akiishi kwa nyumba ya kodi ya shii ngi elfu 9 kwa miaka kadhaa, kwani alikuwa na lengo la kufanikisha ndoto yake ya kujenga kijijini kwanza.

Alitamba na kusema kwamba nyumba mpya ambayo amehamia na mchumba wake Ruth K kodi ni shilingi elfu 70 kwa mwezi.

Walihama siku chache baada ya kufanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza na Ruth K mapema mwezi jana.