Mbunge Oscar Sudi aonyesha furaha yake baada ya kukutana na msanii Diamond Platnumz

Sudi alisema alifanya ziara katika bunge la Afrika Mashariki na kukutana na msanii huyo ambaye walionekana wameketi katika sebule kwenye maongezi.

Muhtasari

• Sudi alisema alifanya ziara katika bunge la Afrika Mashariki na kukutana na msanii huyo ambaye walionekana wameketi katika sebule kwenye maongezi.

Oscar Sudi na Diamond
Oscar Sudi na Diamond
Image: facebook

Mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi ameonyesah furaha yake baada ya kukutana na msanii nambari moja ukanda wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz.

Sudi alifichua kukutana na Diamond kwa kuchapisha picha za pamoja kwenye kochi la kifahari na msanii huyo na kudokeza kwamba walikuwa na mazungumzo ya kina kuhusu kuendeleza ukuzaji wa talanta za vijana kaitka ukanda huu.

Sudi alisema alifanya ziara katika bunge la Afrika Mashariki na kukutana na msanii huyo ambaye walionekana wameketi katika sebule kwenye maongezi.

“Kwa hisani ya ziara ya EAC na Tanzania 🇹🇿 Mwanamuziki Diamond Platinumz ; tulijadili maeneo ya kushirikiana kuchunguza mipango ya utafutaji wa Vipaji vya Vijana,” Sudi aliandika pasi na kutoa maelezo Zaidi kuhusu mkutano huo.

Baadhi ya wafuasi wake walimpongeza kwa hatua hiyo lakini wakataka afafanue Zaidi walichokizungumzia na mmiliki huyo wa moja ya lebo yenye ufanisi mkubwa Afrika Mashariki.

“Engineer na Kazi. Kapseret vijana najua watapata kitu mzuri hapa” Stecy Chepkemoi.

“Good work kiongozi...alafu kuna waimbaji wa uasin Gishu visit them also” Sheillah MIbei alisema.

“Nchini Kenya tuna wanamuziki bora zaidi wa kushirikiana kwa ajili ya mipango kama hii. Tuna Nameless na Wahu. Wasomi sana, wamefichuliwa sana na wana maadili mema kwa hiyo ni washauri wazuri” Emily Sinato.