Pawpaw: Muigizaji mkongwe wa Nollywood aeleza anavyohisi kutumiwa kama meme

Inasemekena karibia kila hali na tukio duniani lina meme ya kulichagiza zaidi kwa njia ya utani. Pawpaw ana umri wa miaka 42 na urefu wa futi 4. Ni maarufu kutokana na filamu ya 'Aki na Pawpaw'.

Muhtasari

• Osita alianza kazi yake ya uigizaji akicheza majukumu madogo kama mtoto katika sinema za Nollywood.

• Mnamo mwaka wa 2002, alikua maarufu nchini Nigeria baada ya kucheza Pawpaw pamoja na Chinedu Ikedieze katika vichekesho vya Aki na Ukwa.

Pawpaw
Pawpaw
Image: Screengrab, maktaba

Muigizaji mkongwe wa filamu za Nollywood kutoka Nigeria, Osite Iheme maarufu kama Pawpaw amefichua jinsi anavyohisi kuona picha na video zake zikitumiwa mitandaoni kama meme za vichekesho.

Inasemekana kwamba Pawpaw mwenye umri wa miaka 42 ambaye anafahamika na wengi kutoka kwa mfululizo wa filamu za ‘Aki na Pawpaw’ Zaidi ya miaka 20 iliyopita, hakuna tukio lisilo na meme ya ama picha yake au video.

Akizungumza na mwanablogu mmoja, Pawpaw kwa mara ya kwanza alifunguka jinsi anavyohisi kuona kila tukio likichagizwa Zaidi na meme ya sura yake.

Kulingana na nyota huyo mkongwe wa sinema, anajisikia vizuri kujiona kila mahali. Alisema ina maana kazi zake zimefanya vizuri na watu wanamkubali japo sinema hizo ni za miaka mingi iliyopita.

Kwa maneno yake: "Ninajisikia vizuri. Ni vizuri kuona kwamba kazi zako zinafanya vizuri huko nje na watu wanathamini kile unachofanya ingawa ni miaka mingi, watu bado wanathamini sasa, kwa hivyo ni nzuri. Inaonyesha kuwa una mali kwa sababu ukiangalia kazi ulizofanya miaka 20 iliyopita, watu bado wanaitumia sasa kujieleza kwa hiyo najisikia furaha.”

Pawpaw anachukuliwa kuwa mmoja wa waigizaji maarufu wa Nigeria. Katika hali nyingi, anafanya kama mtoto mkorofi na mhusika wa kuchekesha.

Pawpaw amekonga nyoyo za mashabiki wengi kutokana na ustadi wake wa kuigiza. Ameleta vicheko kwenye nyuso za watu wengi kwa muda mrefu.

Osita alianza kazi yake ya uigizaji akicheza majukumu madogo kama mtoto katika sinema za Nollywood.

Mnamo mwaka wa 2002, alikua maarufu nchini Nigeria baada ya kucheza Pawpaw pamoja na Chinedu Ikedieze katika vichekesho vya Aki na Ukwa.

Osita Iheme na Chinedu Ikedieze waigizaji katika filamu ya Aki na Ukwa ya 2002 bado inazungumzwa sana.

Wamekuwa wakivuma kupitia meme kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, jambo ambalo limewafanya wawe na mashabiki wengi duniani.