Mwigizaji mbilikomo wa Nigeria, Aki afunguka jinsi aligundua yeye ni mbilikimo

Aki ambaye ameigiza kwa zaidi ya miaka 20 ana umri wa miaka 45 lakini anaonekana kama mtoto mwenye urefu wa futi 4 na inchi 5.

Muhtasari

• Muigizaji huyo maarufu hata hivyo alitaja mchango mkubwa wa mamake kwa ukujai wa ujasiri wake.

Aki na Pawpaw
Aki na Pawpaw
Image: Instagram

Mwigizaji wa muda mrefu aliyeshabikiwa kutoka Nigeria Chinedu Ikedieze almaarufu kama Aki amefunguka kwa ujasiri kuhusu jinsi anahisi anapoona watu wanafanya dhihala kuhusu kimo chake cha mbilikomo.

Aki ambaye amekuwa akiiiza kwa muda mrefu katika filamu za Nigeria na kijana mwengina Pawpaw ambao wote wana muonekano wa mbilikimo licha ya kuwa na umri mkubwa alifunguka hayo katika mahojiano ya hivi majuzi na mwanahabari mmoja kwa jina Chude.

Aki mwenye umri wa miaka 45 alisema kwamba mara ya kwanza kugundua kuwa yeye ni mbilikomo ni pale alipoona ndugu yake mdogo amekua na kumpita kwa urefu, hapo ndipo alijua kwamba huenda kuna tatizo na mwili wake.

Alisema kwamba ndugu yake alimpita kwa urefu akiwa na umri wa miaka 6 tu.

“Katika umri wa miaka 6, nilijua kwamba kulikuwa na tatizo na mwili wangu baada ya kugundua kwamba kakangu mdogo alikuwa amenipita kwa urefu.”

Alikwenda mbele kufunguka kwa ujasiri changamoto ambazo amezipitia katika familia yake wakati anakua, akisema kwamba wakati wa mzozo na ndugu zake, wangemdhihaki kwa kumuita kwa utani jina ambalo watoto wengine walikuwa wanamtania nalo.

“Kwa wakati mwingi tulipokuwa tukitofautiana na ndugu zangu, wangetumia jina la utani ambalo watoto wengine wangenidhihaki nalo,” Aki alisema.

Muigizaji huyo maarufu hata hivyo alitaja mchango mkubwa wa mamake kwa ukujai wa ujasiri wake.

“Mamangu angeniambia muda wote, ‘unajua wewe ni mdogo, huwezi enda na kuanza kubeba mifuko ya simiti ama kusema unataka kuwa seremala, unajua huwezi hilo kutokana na umbilikimo wako, kwa hiyo kitu kizuri kwako ni kuzingatia masomo.’ Kwa hiyo nilijua zana moja ambayo ningejihami nayo ni kufukiza kichwa change vitabuni,” Aki alisema.

Chinedu Ikedieze, MFR, anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Aki, alizaliwa mnamo Desemba 12, 1977 huko Bende, Jimbo la Abia, Nigeria. Yeye ni mwekezaji, mfanyabiashara, na mwigizaji kutoka Nigeria. Ushirikiano wake mashuhuri zaidi wa uigizaji na Osita Iheme ulikuja kufuatia uigizaji wao bora katika filamu ya 2002 Aki na Ukwa.

Ana kimo cha futi 4 na inchi  5  (1.35m)