Jambo la kipumbavu zaidi nimewahi fanya maishani ni kujichubua - muigizaji wa kike ajuta

Mmoja alimuuliza ikiwa angepata nafasi ya kurudisha muda nyuma, ni jambo au kitu kipi ambacho angejutia kukifanya zama hivyo.

Muhtasari

• Chapisho lake, ambalo lilipata mvuto kwenye mitandao ya kijamii, lilizua taharuki huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakishiriki mawazo yao kupitia sehemu ya maoni.

Mrembo ajutia kujichubua.
Mrembo ajutia kujichubua.
Image: Instagram

Mwanahabari maarufu na mwigizaji wa Nollywood Toke Makinwa amefichua kuwa majuto yake pekee katika maisha ni kuchubua rangi ya ngozi yake.

Mtangazaji huyo kupitia ukurasa wake wa X, zamani jukwaa hilo likijulikana kama Twitter alifungua nafasi kwa mashabiki wake kumuuliza kitu chochote huku akiahidi kutoa jibu sahihi bila kubeta.

Mmoja alimuuliza ikiwa angepata nafasi ya kurudisha muda nyuma, ni jambo au kitu kipi ambacho angejutia kukifanya zama hivyo.

Makinwa alifichua kwamba hana kikubwa cha kujutia lakini akasema pengine kama angehitajika kujuta basi ni kuchubua rangi ya ngozi yake, akiita hatua hiyo kuwa jambo la kipumbavu Zaidi ambayo aliwahi chukua.

Mtumiaji @DoyinS oextra, aliandika, "Ikiwa unaweza kurudi nyuma, ungefanya nini tofauti?

Aliandika, "Hakuna. Majuto yanachosha sana!!!! Subiri, labda kuchubua ngozi yangu, lilikuwa jambo la kipumbavu zaidi na ninashukuru sana kwa jeni nzuri na pesa, vinginevyo…”

Chapisho lake, ambalo lilipata mvuto kwenye mitandao ya kijamii, lilizua taharuki huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakishiriki mawazo yao kupitia sehemu ya maoni.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

“Asante kwa kushiriki, watu hawajui jinsi inavyoweza kuharibu ngozi na viungo vyao vya ndani,” Uncle Green.

“Heshima kwa hili. Natumai watu wengi watajifunza kutokana na hili.,” Dice of Truth.

“Kisha uache, ukiishamaliza na kupata chenye ulitaka, unapaswa kuibatili; sababu pekee bado una ngozi nyepesi ni kuwa bado unaifanya,” Oluwafisayo.

“Hii ni nzuri sana kutoka kwako, tunatumai wengine wataona hii na kujifunza kabla haijachelewa,” Olivia Sose.

“Lmaoooo, Kukubali kwenye twitter kuwa ulipauka ngozi yako ni hatua mbaya. Nakutumia kumbato nyingi maana watakapoikumbuka huko mbeleni wataitumia kukuchamba,” Chief Rukkus.