Davido azindua Kitivo cha Muziki na Sanaa katika chuo cha nchini Uganda

Akizindua ukumbi huo, mwimbaji huyo alionekana akikata utepe wa sherehe uliounganishwa kwenye ubao unaoonyesha jina la kitivo kipya, kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kozi hiyo.

Muhtasari

• Kufuatia tangazo hilo, bosi huyo wa 30bg aliwasisimua mashabiki wake kote ulimwenguni, habari hizo ziliposambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

DAVIDO
DAVIDO
Image: Instagram

Mwimbaji aliyeteuliwa kuwania tuzo za Grammy, Davido kutoka Nigeria, anayejulikana kwa umahiri wake wa kisanii amezindua kozi mpya ya ‘Kitivo cha Muziki na Sanaa’ katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Mashariki (IUEA) jijini Kampala, Uganda.

Katika hafla kubwa iliyofanyika chuoni hapo, Davido pia alitunukiwa tuzo maalum yenye maandishi, ‘Davido Hall’ ikiashiria kuwekwa wakfu kwa jumba jipya lililojengwa kwa heshima yake kwenye kampasi ya chuo kikuu.

Kufuatia tangazo hilo, bosi huyo wa 30bg aliwasisimua mashabiki wake kote ulimwenguni, habari hizo ziliposambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizindua ukumbi huo, mwimbaji huyo alionekana akikata utepe wa sherehe uliounganishwa kwenye ubao unaoonyesha jina la kitivo kipya, kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kozi hiyo.

Mwimbaji huyo wa ‘Unavailable’ hivi karibuni alikuwa nchini Uganda ambapo alizindua kitivo cha muziki na sanaa katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Mashariki, jijini Kampala, Uganda.

Uzinduzi huo ulifanyika Alhamisi, Machi 28, 2024.

Kulingana na ripoti zaidi, kitivo hicho pia kitakuwa na idara mpya za media na burudani. Davido mwenye furaha hakuweza kuficha furaha yake katika kuzindua kitivo hicho.

Nyota huyo wa muziki alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Babcock, ambapo idara ya muziki iliundwa alipojiunga na taasisi ya kibinafsi ya elimu ya juu. Alihitimu mnamo Julai 2015, na digrii ya muziki baada ya babake kulipia chuo kikuu kuanzisha idara ya muziki kwa darasa la uzinduzi la mwanafunzi mmoja.

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Mashariki ni taasisi ya kibinafsi isiyo ya faida nchini Uganda. Pia ni Chuo Kikuu kilichokodishwa na Baraza la Kitaifa la Uganda la Elimu ya Juu.