Babake msanii Mohbad aeleza sababu za kuendelea kuvaa nguo za marehemu mwanawe (video)

Mzee huyo anasema kuwa mwili wake ni sawa na mtoto wake marehemu Mohbad na kuvaa nguo zake baada ya kuaga dunia ni njia ya kuonyesha jinsi alivyompenda na anazidi kumuenzi.

Muhtasari

• Kumbuka kwamba mwimbaji huyo aliyeaga dunia Septemba 12 mwaka jana, alizikwa siku iliyofuata, Septemba 13.

• Kufuatia utata wa kifo chake, uchunguzi wa maiti ulitakiwa na Wanigeria na mwili wake ukafukuliwa Septemba 21.

Mohbad na babake
Mohbad na babake
Image: Screengrab

Joseph Aloba, baba wa marehemu mwimbaji wa Nigeria Mohbad katika mahojiano ya hivi majuzi alifichua kwa nini huwa anavaa nguo za marehemu mwanawe.

Watumiaji wa mtandao wamekuwa wakimlaumu mzee huyo kwa kurithi na kuvaa nguo zote za kibunifu za marehemu mwanawe.

Akijibu shutuma hizo zote, baba wa Mohbad anathibitisha kwamba huwa anavaa nguo za marehemu mwanawe akisisitiza kuwa Mohbad alikuwa mwanawe na kwa kuongeza anaweza kuvaa nguo zake.

Mzee huyo anasema kuwa mwili wake ni sawa na mtoto wake marehemu Mohbad na kuvaa nguo zake baada ya kuaga dunia ni njia ya kuonyesha jinsi alivyompenda na anazidi kumuenzi.

Aliongeza kuwa mtu yeyote ambaye hapendi anavyovaa nguo za marehemu mtoto wake ana uhuru wa kusema chochote anachopenda kwani lengo lake pekee kwa sasa ni kupata haki kwa marehemu mtoto wake Mohbad.

Kwa maneno yake; “Mohbad ni Mwanangu naweza kuvaa Nguo zake, wote tunavaa Nguo kiwango sawa, Yeyote asiyependa kuvaa nguo za Marehemu mwanangu ana uhuru wa kusema chochote apendacho, Focus yangu pekee sasa hivi ni Kupata Haki kwa Marehemu Mwanangu.”

Kumbuka kwamba mwimbaji huyo aliyeaga dunia Septemba 12 mwaka jana, alizikwa siku iliyofuata, Septemba 13.

Kufuatia utata wa kifo chake, uchunguzi wa maiti ulitakiwa na Wanigeria na mwili wake ukafukuliwa Septemba 21.

Hata baada ya uchunguzi kukamilika, baadae iliarifiwa kwamba babake alikataa kuuchukua mwili kwa ajili ya maziko upya, jambo ambalo lilichukua muda mrefu kwa Mohbad kuzikwa tena.