Jackie Chan awatoa wasiwasi mashabiki kuhusu picha yake akiwa mnyonge na mzee!

Jackie Chan ambaye alifikisha umri wa miaka 70 siku tatu zilizopita alifichua kwamba amekuwa kwenye tasnia ya kutengveneza sinema kwa miaka 62, hivyo kila mara yeye hupenda kujaribu kuigiza kama mhusika tofauti.

Muhtasari

• Chan alisema kwamba yeye bado yu mzima wa afya na kujivunia kufikisha umri huo huku akikumbuka nukuu ya kakake mkubwa kuhusu kukua hadi kufikia uzeeni.

• Mkongwe huyo alifichua kuwepo kwenye tasnia ya filamu kwa miaka 62 na alipitia baadhi ya picha zake na kuzichapisha akivuta kumbukumbu za mashabiki wake wa tangu zaman

JACKIE CHAN,
JACKIE CHAN,
Image: FACEBOOK//JACKIE CHAN

Muigizaji mkongwe wa filamu za sarakasi na kupigana, Jackie Chan hatimaye amevunja kimya kuhusu picha iliyowapa wasiwasi sehemu ya mashabiki wake wakitilia shaka afya yake.

Mkongwe huyo ambaye amethibitisha kufikisha umri wa miaka 70 hivi majuzi alisema kwamba picha hiyo ambayo ilivujishwa mtandaoni ikimuonyesha mwenye mvi na unyonge wa uzee ilikuwa ni muonekano wake katika filamu mpya aliyoigiza na ambayo haijatoka.

“Sio muda mrefu uliopita, marafiki wengi waliona picha zangu za hivi karibuni kwenye mtandao, na wote walikuwa na wasiwasi kuhusu afya yangu. Ninataka kuchukua fursa hii kuwajulisha kila mtu, msijali! Ni mwonekano wa mhusika wa filamu yangu mpya zaidi. Tabia inanihitaji niwe na nywele nyeupe, ndevu nyeupe na nionekane mzee,” Chan alisema.

“Kwa miaka mingi, nimekuwa tayari kujaribu vitu vipya kwa ajili ya filamu, haijalishi ikiwa ni shida au mwonekano wa mafanikio kwa mhusika. Nimekuwa katika biashara ya burudani kwa miaka 62 na ninathamini kila wakati kwa sababu nina bahati bado ninarekodi leo.”

Chan alisema kwamba yeye bado yu mzima wa afya na kujivunia kufikisha umri huo huku akikumbuka nukuu ya kakake mkubwa kuhusu kukua hadi kufikia uzeeni.

Mkongwe huyo alifichua kuwepo kwenye tasnia ya filamu kwa miaka 62 na alipitia baadhi ya picha zake na kuzichapisha akivuta kumbukumbu za mashabiki wake wa tangu zamani.

“Hivi majuzi wafanyikazi wangu wamekuwa wakipitia kumbukumbu zangu za picha na kupata picha nyingi za kukumbukwa. Nimechagua chache wa kuchapisha na ujumbe huu. Kuangalia picha hizi kunarudisha kumbukumbu nyingi za kupendeza. Ninachoweza kusema ni: Ninapenda kutengeneza sinema na ninawapenda nyote.”

“Asante sana kwa kila mtu kwa matakwa yako yote ya siku ya kuzaliwa. Natumai kila mtu atakuwa na furaha na afya!” alimaliza Chan.

Muigizaji na muongozaji wa sinema huyo kutoka Hong Kong alichukua safari ya kwenda chini kwenye njia ya kumbukumbu na kutafakari juu ya safari yake ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 70 Jumapili, Aprili 7, 2024.