Mrembo mcheza densi wa Nigeria ashambuliwa kwa visu na asidi nchini UK akifanya live-streaming

Obidi ambaye alithibitisha tukio hilo la kutishia maisha kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema mwanamke mweusi mrefu alimvizia na kumchoma kisu kabla ya kummwagia asidi usoni wakati akifanya live streaming.

Muhtasari

• Katika nukuu iliyoambatana na video hiyo ya kutatanisha, Obidi aliomba umma kwa taarifa yoyote ambayo inaweza kumtambua na kumkamata mshambuliaji wake.

KORRA OBIDI
KORRA OBIDI
Image: Instagram

Mrembo anayefahamika kwa uchezaji wake wa densi kutoka nchini Nigeria, Korra Obidi amedai kushambuliwa kwa visu na kumwagiwa asidi wakati akitiririsha video ya kujirekodi ya moja kwa moja akiwa nchini Uingereza.

Obidi ambaye alithibitisha tukio hilo la kutishia maisha kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema mwanamke mweusi mrefu alimvizia na kumchoma kisu kabla ya kummwagia asidi usoni wakati akifanya live streaming.

Katika nukuu iliyoambatana na video hiyo ya kutatanisha, Obidi aliomba umma kwa taarifa yoyote ambayo inaweza kumtambua na kumkamata mshambuliaji wake.

Akielezea mshambuliaji, Obidi alisema alikuwa mwanamke Mweusi mwenye urefu wa futi tano. Aidha alifichua kuwa aliwahi kukabiliwa na maoni ya chuki mtandaoni hapo awali, lakini shambulio hili la kimwili linatumika kama ujumbe wa kumuamsha.

“Hivi sasa nikiwa kwenye gari la wagonjwa kuelekea hospitalini, nilipata shambulio la kisu, tindikali nchini Uingereza 🇬🇧 katikati ya mtiririsho wa moja kwa moja. Kumekuwa na chuki nyingi huko nyuma lakini shambulio hili la kimwili ni simu ya kuamsha. Ikiwa una habari yoyote kuhusu mshambuliaji, mwanamke mweusi mwenye futi tano nijulishe,” aliandika.

“Jamani niko hospitalini. Usalama wakati wa usafiri sio jambo lisilo la lazima tena bali ni lazima. Asidi ilikuwa salicylic na nilikuwa na bahati. Nawapenda nyie,” aliongeza.

Picha za mtiririko wa moja kwa moja ziliripotiwa kumuonyesha Korra Obidi akiwa katika dhiki, akiosha uso wake kwa jazba kwa kinywaji cha Coca-Cola, uwezekano wa kupunguza hisia inayowaka ya shambulio la asidi.

Maafisa wawili waliovalia sare walifika eneo la tukio, walinaswa kwenye video. Afisa mmoja alimpaka usoni kiowevu, labda ili kupunguza maumivu. Afisa mwingine anaweza kuonekana akinyunyiza mgongo wake, ikiwezekana kutoa huduma ya kwanza.