Davido achangamsha mioyo ya mashabiki kwa kumzawadia shabiki wa kike Ksh 6.7m (Video)

Mrembo huyo alisema uwa alikuwa anahitaji angalau dola laki moja (Ksh 13.25m) na Davido akamuita msaidizi wake na kumtaka kumkabidhi mrembo huyo dola elfu 50 (Ksh 6.63m) taslimu ili kutatua shida yake.

Muhtasari

• Shabiki huyo wa kike alihamaki alipotoa shukrani zake kwa Davido wakati akitoka nje ya jukwaa

Davido azungumzia kupata mapacha.
Davido azungumzia kupata mapacha.
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Afrobeat wa Nigeria, David Adeleke, almaarufu Davido, amenyoosha mikono yake mikarimu kwa shabiki wa kike wa Marekani wakati wa shoo yake iliyofanyika Madison Square Garden (MSG) jijini New York hivi majuzi.

Kutokana na video moja kutoka kwa tukio hilo, mrembo huyo alionekana na bango akiwa anaomba msaada wa kulipa bili zake.

Davido ambaye alikuwa anatumbuiza albamu yake ya Timeless kwenye ukumbi huo weney uwezo wa kubeba mashabiki walioketi 19,500 aliona bango la shabiki huyo aliyekuwa katika nafasi ya mbele kabisa karibu na jukwaa.

Hit maker huyo mwenye umri wa miaka 31 alichukua bango lile kutoka kwa mrembo huyo kabla ya kumuita kupanda jukwaani na kumsogezea kipaza sauti akimuuliza deni la bili yake ya karo ya shule.

Mrembo huyo alisema uwa alikuwa anahitaji angalau dola laki moja (Ksh 13.25m) na Davido akamuita msaidizi wake na kumtaka kumkabidhi mrembo huyo dola elfu 50 (Ksh 6.63m) taslimu ili kutatua shida yake.

Shabiki huyo wa kike alihamaki alipotoa shukrani zake kwa Davido wakati akitoka nje ya jukwaa.

Mashabiki na wapenzi wa muziki walimshangilia Davido kwa kitendo chake cha fadhili kwa mwanadada huyo. Baadhi ya majibu yanaonyeshwa hapa chini:

jully__mk alisema, “Nitasema tena! Sijaona Msanii anayeweza kufanya kama Davido! ❤”.

ma_vins626 alisema, "Fanya wizkid ajaribu kuonyesha kazi 😂😂, na ni yeye tu anayemshabikia".

danzy_010 alisema, "Na hivyo wanawake Davido wanatoa pesa 😂😂".

markzuco200 alisema, "Omo lakini kwa nini mtu aende kukopa 100k  kutoka USA department kwa ajili ya shule tu 😂😂".

henny_sucks alisema, "Hawezi saidia Wanaijeria wenzake na sapoti kubwa wanayompa hapa".