Karen Nyamu afurahia AI ikifanya video yake akitumbuiza kama msanii kwa umati wa mashabiki

Nyamu kupitia Instagram yake alipakia video hiyo ikionyesha picha iliyoasisiwa na akili mnemba kama yeye kwenye vazi la samawati na wigi lake akitembea kuelekea jukwaani kabla ya kuanza kutumbuiza.

Muhtasari

• “Mnanizoea sana…na hapa nyuma mmenifanyia udhalimu,” Nyamu alinukuu video yake ya AI alipokuwa akichangamka kwenye midundo ili kusawazisha.

Karen Nyamu ashangazwa na video yake ya AI
Karen Nyamu ashangazwa na video yake ya AI
Image: Screengrab

Seneta maalum wa Nairobi, Karen Nyamu ameonesha furaha yake baada ya kukutana na video ya akili mnemba ikimuonesha akitumbuiza kama msanii kwenye jukwaa lililofurikwa na mashabiki.

Nyamu kupitia Instagram yake alipakia video hiyo ikionyesha picha iliyoasisiwa na akili mnemba kama yeye kwenye vazi la samawati na wigi lake akitembea kuelekea jukwaani kabla ya kuanza kutumbuiza akiwarushia mashabiki mikono.

Katika video hiyo, alisema kwa mzaha kuwa watu walikuwa wakimpenda hivyo basi kuhariri video hiyo ili kumfaa. Alibainisha kuwa watu walimtendea isivyo haki huku akiongeza emoji za kucheka mwishoni.

“Mnanizoea sana…na hapa nyuma mmenifanyia udhalimu,” Nyamu alinukuu video yake ya AI alipokuwa akichangamka kwenye midundo ili kusawazisha.

Mashabiki wake walimuasa kuchukua fursa hiyo na kujiongeza kwa Sanaa kando na siasa.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake kwenye Instagram;

“Ila unaendelea vizuri sana.😂😂😂” k_jeff.

“Mlisema hii Kenya hakuna kupumzika 😂😂😂😂” njeri7664.

“Wow...2027 hivi ndio utakua unajaza kasarani...mungu mbele”micmasmbutu.

Tazama video hiyo hapa;