MP Salasya aeleza kwa nini alimsherehekea mamake kwa kumnunulia samani za thamani

“Leo nimeamua kumsherehekea kwa namna tofauti kwa kuhakikisha analala kwenye kitanda kizuri na kuhakikisha nyumba yake inaonekana ya kisasa kuliko yangu hehe. Happy mother’s day,” Salasya alisema.

Image: Facebook

Jumapili, wikendi ilisherehekea siku ya kina mama duniani.

Watu mbalibali walichukua kwenye mitandao ya kijamii kusherehekea mama zao wengine wakipakia picha za zawadi na mambo mazuri ambayo wamewafanyia wazazi wao wa kike siku hiyo spesheli kwao.

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya alikuwa miongoni mwa Watu waliopeleka katika mitandao ya kijamii kuwasherehekea kina mama siku yao.

Salasya alipakia picha ya pamoja na mamake na baadhi ya zawadi ambazo alimpa kumthamini siku hiyo kuu.

Mbunge huyo mcheshi alimnunulia mamake samani za thamani zikiwemo kitanda, viti na meza na hakusita kutoa sababu kwa nini aliamua kufanya hivyo.

Kwa mujibu wake, alitaka kumfanya mamake kujihisi wa fahari Zaidi na kurembesha nyumba yake, Zaidi hata kuliko nyumba yake mwenyewe.

“Leo nimeamua kumsherehekea kwa namna tofauti kwa kuhakikisha analala kwenye kitanda kizuri na kuhakikisha nyumba yake inaonekana ya kisasa kuliko yangu hehe. Happy mother’s day,” Salasya alimuandikia mamake.

Siku ya kina Mama huadhimishwa kila mwaka Jumapili ya pili ya Mei; kwa hivyo, tarehe inabadilika kila mwaka.