“Kusema ukweli hiyo siku hatukuwa tumekula!” Simple Boy kuhusu kuanguka stejini 10/10

“Kusema ukweli hiyo siku hatukuwa tumekula, wacha nieleze kidogo, kusema ukweli hiyo siku hatukuwa na kakitu, na kulikuwa na kiporo Fulani kilikuwa kimebaki,” Stevo alisema kabla ya kukatishwa na Chingiboy.

Muhtasari

• “Stevo, subiri, kusema tu ukweli, hiyo Ijumaa si mimi ndio nilipika?” Chingiboy alimuuliza Stevo kwa nia ya kumwonyesha kuwa alikuwa anajichanganya katika maelezo yake.

• Kisha Stevo akamjibu Chingiboy akisema kwamba ni kweli kulikuwa na kitoweo lakini ugali ulikuwa tu ni ule wa jana uliobaki wala si wa hiyo siku.

Stevo Simple Boy
Stevo Simple Boy
Image: Facebook

Kwa mara ya kwanza, msanii Stevo Simple Boy amefafanua kuhusu tukio la kushangaza lililomkuta wiki chache nyumba baada ya kuanguka na kuzirai stejini akiwa anatumbuiza.

Msanii huyo katika kisa cha kuogofya, alikuwa anatumbuiza kwenye kipindi cha moja kwa moja cha 10/10 kwenye runinga ya Citizen alipodondoka sakafuni ghafla na kuzimia.

Akirejelea tukio hilo wakati wa mkutano wa maridhiano na aliyekuwa meneja wake Chingiboy Mstado ambapo alirudishiwa akaunti zake za mitandao ya kijamii, Simple Boy alisema kwamba hiyo siku hakuwa amekula akienda kutumbuiza.

“Kusema ukweli hiyo siku hatukuwa tumekula, wacha nieleze kidogo, kusema ukweli hiyo siku hatukuwa na kakitu, na kulikuwa na kiporo Fulani kilikuwa kimebaki,” Stevo alisema kabla ya kukatishwa na Chingiboy.

Kwa upande wake, Chingiboy alikanusha madai ya Stevo kwamba hakuwa amekula hiyo siku akijiandaa kuenda katika shoo ya 10/10.

Kwa mujibu wake, hiyo siku yeye ndiye alipika na wakala pamoja na msanii wake.

“Stevo, subiri, kusema tu ukweli, hiyo Ijumaa si mimi ndio nilipika?” Chingiboy alimuuliza Stevo kwa nia ya kumwonyesha kuwa alikuwa anajichanganya katika maelezo yake.

Kisha Stevo akamjibu Chingiboy akisema kwamba ni kweli kulikuwa na kitoweo lakini ugali ulikuwa tu ni ule wa jana uliobaki wala si wa hiyo siku.

“Kulikua na kitoweo lakini kiporo, Ugali,” Stevo alijibu swali la Chingi.

Stevo Simple Boy alikuwa ameanguka jukwaani alipokuwa akitumbuiza kwenye kipindi cha 10/10; kitu ambacho wengi walitafsiri ni stress aliyokuwa nayo Stevo kwa sababu meneja wake alikuwa amemuacha.