Celestine amnunulia Njugush kofia kadhaa kama zawadi za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa

"Jamani nipeeni ideas, nyinyi venye mnajua Kimani nini inaeza mjazz aki. Ama nimbuiye mbolea??” Celestine aliuliza kwa utani.

Muhtasari

• "Jamani nipeeni ideas, nyinyi venye mnajua Kimani nini inaeza mjazz aki. Ama nimbuiye mbolea??” Celestine aliuliza kwa utani.

 

Njugush
Njugush
Image: Instagram

Celestine Ndinda, mkewe mchekeshaji Njugush amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kumnunulia mumewe kofia kadhaa kama zawadi za kumsherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia Instagram, Ndinda alipakia  video wakiwa na Njugush ndani ya nyumba kabla ya kumkabidhi kifurushi kwenye mfuko wa samawati.

Njugush alipotaka kujua kilichokuwemo ndani, Ndinda alimuomba kufungua na kukuta ni kofia kadhaa zilizokuwemo ndani, na kumkumbusha kwamba ni zawadi za siku yake ya kuzaliwa.

“Happy birthday, sasa uko na kofia ya kila siku, mimi nishamalizana na wewe,” Ndinda alimwambia huku Njugush akijipima kila kofia kichwani.

Celestine alidokeza kwamba kofia hizo zilikuwa tano kama siku za wiki, kila moja ikivaliwa kwa siku yake.

“Zawadi 5 za Siku ya Kuzaliwa kwa Bw.Timothy! Kesho ni siku yake ya kuzaliwa!! Unaona kama zawadi hizi zimeweza ama??? Sasa anasubiri zawadi Namba 6😂😂😂. Jamani nipeeni ideas, nyinyi venye mnajua Kimani nini inaeza mjazz aki. Ama nimbuiye mbolea??” Celestine aliuliza kwa utani.

Wanandoa hao wanaoaminika kuanza safari yao ya uchumba wakiwa chuoni mpaka sasa wana watoto wawili na hivi majuzi wamejitosa katika biashara ya uchukuzi wa umma kwa kununua gari lao lenye uwezo wa kubeba abiria 33.