Eric Omondi kutumia mamilioni kwa ‘birthday’ ya kwanza ya bintiye

Hio siku tutatafuta jinsi watu watapewa holiday wasiende kazini

Muhtasari

•Hio siku tutatafuta jinsi watu watapewa holiday wasiende kazini. Kwa sababu yeye ni binti mfalme.

•Kama tutahamua kuwahalika watu wote tutaweka pale Nyayo kila mtu akuje amuone

ERIC OMONDI NA MPENZIWE LYNNE NA MTOTO WAO
Image: instagram

Mchekeshaji Eric Omondi alisema yuko tayari kugharamia karamu kubwa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa kwa bintiye.

Wapenzi hao wawili walimkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja mnamo Agosti 9, 2023.

Eric Omondi sasa asema yuko tayari kumpa bintiye siku ya kuzaliwa yenye thamani ya kukumbukwa.

Omondi alisema kuwa angewapa mashabiki wake likizo siku hio ya kuzaliwa ya bintiye.

‘Hio siku tutatafuta jinsi watu watapewa holiday wasiende kazini. Kwa sababu yeye ni binti mfalme. Yeye ni binti wa Mfalme na Malkia. Kutakua na siku ya kuzaliwa moja Kisumu. Kutakua na injini Murang’a na injini Nairobi.”

Eric alisema kuwa kama sherehe hio hitakuwa ya watu wote inawezekana kuwa ataiweka katika uwanja wa Nyayo.

“kama tutahamua kuwahalika watu wote tutaweka pale Nyayo kila mtu akuje amuone” Eric alielezea.

Hivi majuzi Eric alifichua mipango yake ya kuongeza mabinti zaidi na Lynn.

 Eric alifichua kwamba alifurahi zaidi kupata mtoto wake mwenyewe baada ya kungoja kwa subira kwa miaka 41.