Okoa waathiriwa wa endometriosis' - Jahmby Koikai amrai Ruto anapozuru Marekani

Jahmby ambaye ni mgonjwa wa endometriosis amrai Rais Ruto kutumia ziara yake kuwaokoa waathiriwa wa ugonjwa huo.

Muhtasari

•Atlanta, Georgia ni jiji ambayo ni ndoto kwa kila msichana mdogo na mwanamke ambaye amewahi kupambana na ugonjwa huu mbaya unaoitwa Endometriosis.

•Jahmby ambaye ni mgonjwa wa endometriosis amrai Rais Ruto kutumia ziara yake kuwaokoa waathiriwa wa ugonjwa huo

Mary Njambi Koikai
Image: Fyah Mummah Jahmby Koikai (Facebook)

Mwanahabari Mary Njambi Koikai anayejulikana sana kama Jahmby Koikai ametuma pendekezo ya afya kwa Rais William Ruto ambaye alianza ziara yake ya kitaifa nchini Marekani kwa siku tatu mnamo Jumatatu, 20, Mei, 2024.

Akitumia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Jahmby alimtaka Ruto pia kuzingatia matibabu ya endometriosis kwa kuwa uwekezaji katika afya ni mojawapo ya maeneo muhimu katika ziara yake.

Jahmby, ambaye ni mgonjwa wa endometriosis alieleza kuwa ni shauku kwa wasichana wadogo na wanawake wanaopambana na ugonjwa huo wa kutisha kupata matibabu yanayofaa katika hospitali ya kifahari iliyoko Atlanta Georgia.

“Huu ni wito wa dhati wa msaada kwa viongozi wachache wa Kenya lakini niruhusu nizungumzie hili kwanza na Rais William Ruto anapofanya ziara yake nchini Marekani. Mheshimiwa Rais, moja ya maeneo muhimu katika ziara yako ni uwekezaji katika afya,” alisema.

"Atlanta, Georgia ni jiji ambayo ni ndoto kwa kila msichana mdogo na mwanamke ambaye amewahi kupambana na ugonjwa huu mbaya unaoitwa Endometriosis. Hapo ni kituo kilichojitolea kurejesha maisha ya wasichana na wanawake ambao wamelemazwa na ugonjwa huu. The @centerforendocare,” alieleza.

Alitaja maeneo ambayo angependa Rais Ruto kutembelea hili kuweza kupata ufahamu kuhusu ugonjwa huo na pia zina uwezo wa kuwasaidia wanawake wengi hapa nchini.

"Unapoanza ziara yako ya  nchini Marekani, ningependa utembelee sehemu ambazo zingesaidia mamilioni ya wanawake wa Kenya wanaopigana kimyakimya na ugonjwa huu,vituo kama Huduma ya Endometriosis na kitengo cha Wanawake cha Hospitali ya Northside " alielezea.