Kate Actress:Baadhi yetu hatuhitaji kulipiwa nauli kwenda US

Mwigizaji huyo amesema kuwa alijifadhili mwenyewe kwenye safari yake ya Marekani pasi na kumtegemea yeyote jinsi wengi wafikiriavyo

Muhtasari

•Mwigizaji Kate amefichua kuwa alijifadhili mwenyewe kwenye safari yake ya Marekani

Catherine Kamau
Catherine Kamau
Image: INSTAGRAM

Mwigizaji wa Kenya Catherine Kamau almaarufu Kate Actress amewajibu wakosoaji wanaodai safari yake ya kwenda Marekani inafadhiliwa na pesa za walipa kodi.

 Mwigizaji huyo alimjibu  shabiki mmoja aliyekomenti kwenye picha  yake instagram. '...baadhi yetu hatuhitaji fedha za serikali ili kustawi,safari hii inajifadhili kikamilifu, hii ni mimi kuwekeza kwenye brand yangu na kuzingatia biashara yangu ..Unapaswa kujaribu," alisema Kate .

Kwenye Instagram, Mwigizaji  Kate alisema kwamba safari hiyo inalenga kukuza brandi yake na amejifadhili mwenyewe.Alifafanua kuwa mwaliko wake ulikuwa kwa hisani ya ubalozi wa Marekani.

 Siku zilizopita,mwigizaji huyo aliyeshinda tuzo za mwigizaji bora;alitumia akaunti yake rasmi ya mtandao wa kijamii kufichua mwaliko wake wa kuhudhuria chakula cha jioni cha Jimbo katika Ikulu ya White House na Luncheon kwenye studio maarufu ya Tyler Perry huko Atlanta.

Taarifa hio ilisoma;

”Habari za asubuhi, msichana huyu wa kijijini atahudhuria mlo wa jioni wa Serikali katika Ikulu ya White House na Chakula cha mchana katika Studio za Tyler Perry huko Atlanta kwa mwaliko kutoka kwa Mheshimiwa Balozi Meg Whitman.

Eddie Butita pia yuko Marekani baada ya kuandamana na Rais William Ruto katika ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Marekani.