Pasta Ng'ang'a amkashifu Kanyari kufuatia matendo yake mitandaoni

Ng'ang'a alizungumzia uamuzi wake wa kuondoka TikTok, akihusisha mtandao huo na dharau miongoni mwa watumiaji.

Muhtasari

•Mchungaji James Ng'ang'a alimkosoa waziwazi nabii Victor Kanyari kwa tabia yake ya kutatanisha mtandaoni iliyosababisha hasira ya umma.

•Mchungaji Ng'ang'a alitilia shaka kukosekana kwa maendeleo katika huduma ya Kanyari, akibainisha kuwa bado hana kanisa licha ya miaka ambayo imepita.

Image: HISANI

Mhubiri James Ng'ang'a amemkashifu nabii Victor Kanyari kufuatia matukio yake ya hivi majuzi kwenye mtandao wa tiktok  ambayo yalizua utata na kuibua gumzo miongoni mwa umma.

Akizungumza wakati wa mahubiri katika kanisa lake la Neno Evangelism Centre, Ng'ang'a alitoa matamshi yake yaliyoonekana kumlenga mhubiri huyo mwenzake.  

Mhubiri huyo alisema aliacha  kutumiaTikTok kwa sababu ya watu wasio na adabu ambao wanatumia mtandao huo.  

"Niliondoka TikTok baada ya kuona takataka kutoka kwa viumbe hawa. Kwa nini wahubiri hawa hawakufi?"

Alisema kuwa anaomba sana Mungu alete mafuriko pamoja na radi ili kuwaadhibu watu ambao wanafanya makosa kwa kizazi hiki.

“Natamani sana Mungu alete radi itupige sisi wote pia mimi kama niko miongoni mwao kwa sababu jinsi watu wanavyoenda kiholela na kumkosea Mungu na hiki kizazi kibaya” aliongezea.

Aliendelea kubainisha jinsi alivyohubiri katika kanisa hiyo ya Kanyari na kudai bado hajabadilika na hakuna maendeleo amefanya tangu wakati huo.

 "Nilihubiri katika eneo lake nilipofika Nairobi, yeye alikuwa Kawangware, na mpaka sasa, bado yuko huko bila kanisa ikiwa haujamaliza mambo ya kidunia, kaa huko, usichanganye haya mambo mawili Miaka yote hii na hana hata kanisa, lile la Kamulu, eneo la Mkuru. Nilimuacha pale na bado yuko palepale.” Mchungaji Ng’ang’a pia alisema.

Alisema afadhali yeye aende mbinguni uchi na bila utajiri wowote lakini akuwe na wokovu.