Truth WatchDog afunguka kuhusu mamake kumtelekeza akiwa mtoto

Alidai alikuwa na miaka 3 pekee wakati mamake alipoondoka na hivyo hawezi kukumbuka sura yake.

Muhtasari

•Kando na kuzungumzia masomo yake hadi alipojiunga na tasnia ya burudani, Truth Watchdog pia iliangazia maisha yake ya utotoni.

•Aliendelea kufichua kuwa baada ya kuondoka hapakuwa na mawasiliano kati yake na yeye hivyo kumbukumbu kufifia.

Image: INSTAGRAM// TRUTH WATCHDOG

Mtayarishaji wa maudhui Truth watch dog amejitokeza na kuzungumzia maisha yake mbali na kazi yake ya mtandaoni ambayo Wakenya wengi wamemjua nayo.

Kando na kuzungumzia masomo yake hadi alipojiunga na tasnia ya burudani, Truth Watchdog pia iliangazia maisha yake ya utotoni akifichua uhusiano mbaya na mama yake.

Alisema kwamba mama yake aliwaacha wakiwa watoto, baba yake na kaka zake. Alisema mama aliondoka na dada yao mdogo miaka 31 iliyopita.

“Sijui chochote kuhusu mama yangu, ninachojua ni kile nilichoambiwa. Fanya hesabu, miaka 31 iliyopita na sasa nina miaka 34. Sikumbuki chochote kuhusu mama yangu,” Truth Watch Dog alisema.

Wakati mamake akiondoka, Truth Watchdog alisema alikuwa na umri wa miaka 3 pekee na hawezi kukumbuka jinsi mama yake alivyokuwa au sababu iliyomfanya aamue kumwacha licha ya umri wake mdogo.

Aliendelea kufichua kuwa baada ya kuondoka hapakuwa na mawasiliano kati yake na yeye hivyo kumbukumbu kufifia.

Akiwa na miaka 15 walijaribu kurekebisha uhusiano wake na mama hata hivyo haikuwezekana na hadi leo hajawai kumuona.

Alidai kuwa baba yao mzazi aliwauza baada ya mama kuenda  ili kupunguza shida na kufanya yeye  kutengana na ndugu yake.