Dem wa facebook na obinna wakosoa mavazi ya simpleboy

Anafanya vizuri kingoma, but mahali imefika kama Stevo SimpleBoy anahitaji advisor pastor ama Mnigeria.

Muhtasari

•Huwa nahisi kama kuna mzee ameishi ndani ya Stevo na ako na misemo na methali, na kwamba mzee anajitahidi kutoka.

•Na simpleBoy ni kama ni comedian ni kama hii ya kuimba tunamlasimisha talanta ako na misemo mingi sijui matulinga mara shega.

Obinna and Dem wa facebook
Image: facebook

Watayarishaji wa maudhui nchini Kenya Dem wa facebook na Obinna wamekosoa mavazi mapya ya Stevo Simple Boy.

Wakizungumza wakati wa onyesho la kila wiki na Obinna, Dem Wa Facebook alisema kuwa msanii huyo anafanya vyema kimuziki lakini anaharibu sura yake kwa kuvaa kile alichokitaja kama ‘Kanzu za red’.

“Anafanya vizuri kingoma, but mahali imefika kama Stevo SimpleBoy anahitaji advisor pastor ama Mnigeria. Amevaa kanzu za red amehang ndani alafu amefungua kitu cha kichwa anakaa.” Dem Wa facebook alisema.

Dem Wa Facebook alipendekeza kuwa Stevo avae nguo za maana akisisitiza tu kwamba mwonekano mpya ya Stevo inamfanya aonekane wa ajabu na anapaswa kufikiria kujaribu kitu kingine.

Obinna, kwa upande wake, alisema kuwa siku zote anahisi kama kuna mzee anayeishi ndani ya mwili wa Stevo Simple Boy, ndiyo maana yuko jinsi alivyo.

“Ninachotaka kusema kinatoka mahali pazuri moyoni mwangu huwa nahisi kama kuna mzee ameishi ndani ya Stevo na ako na misemo na methali, na kwamba mzee anajitahidi kutoka. Juu ukiangalia stevo vizuri anakaa mchanganyiko ya mtu mzee na kijana mdogo.” Obinna alisema.

Anaendelea kuongeza kuwa Stevo anaweza kutengeneza mcheshi mzuri kwa sababu misemo zake nyingi za kuchekesha ambazo mara nyingi hunukuu akisema kuwa zinaweza kumlazimisha kufanya kitu ambacho hapendi.

“Na simpleBoy ni kama ni comedian ni kama hii ya kuimba tunamlasimisha talanta ako na misemo mingi sijui matulinga mara shega."