Ringtone asimulia matatizo yaliomkumba baada ya akaunti zake za benki kufungwa

Ukiwa nayo watu wanakupenda lakini ukikosa wanakucheka lakini uzuri maisha ni kupanda na kushuka

Muhtasari

•Haya yalitokea miezi michache nyuma baada ya taasisi ya serikali kumzuia kupata pesa zake kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili mahakamani wakati huo.

•“Nilikuwa nikikabiliwa na changamoto za maisha nilipitia magumu na kupoteza furaha yangu.” Ringtone alisimulia.

Ringtone.
Ringtone.
Image: Instagram

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Ringtone, akizungumza wakati wa mahojiano,  alifunguka kuhusu maisha haliyoishi baada ya akaunti zake za benki kufungwa.

Inaonekana haya yalitokea miezi michache nyuma baada ya taasisi ya serikali kumzuia kupata pesa zake kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili mahakamani wakati huo.

“Nilikuwa nikikabiliwa na changamoto za maisha nilipitia magumu na kupoteza furaha yangu.” Ringtone alisimulia.

 Kulingana na Ringtone hakuweza kupata chochote kutoka kwa akaunti yake ikimaanisha sasa alilazimika kuanza kuishi kwa kukula avocado kutoka kwa boma lake kwani hakuwa na uwezo wa kumudu chochote.

“Kuna wakati nilikua na shida zangu mwenyewe lakini nashukuru mungu amenitoa kwa hio kuna wakati nilikosa hadi chakula nilikula avocado asubuhi,lunch na supper juu hizo avocado kwangu zimemea zinaanguka,” alisema.

Aliendelea kuongezea kuwa amejifunnza mengi wakati huo alikuwa na matatizo kwa sababu watu wanakupenda wakati huko na mafanikio lakini ukikosa wanakucheka.

“Ukiwa nayo watu wanakupenda lakini ukikosa wanakucheka lakini uzuri maisha ni kupanda na kushuka,” alisema.

Hata hivyo miezi kadhaa baadaye anaonekana kurejesha akaunti zake na amerejea kwenye maisha yake ya kawaida mtandaoni.