Nilikuwa mchuuzi kabla ya pesa na umaarufu, Ringtone asema

Ringtone alikuwa mtu kawaida tu aliyehangaika kutafuta riziki kabla ya pesa na umaarufu wake

Muhtasari

•Akizungumzia utajiri wake, Ringtone alikiri kwamba kabla ya pesa na umaarufu sio wanawake wengi walikua wanamtaka.

Ringtone.
Ringtone.
Image: Instagram

Rightone amesema kazi ya uchuuzi haswa wa CD za muziki na filamu ni kazi ambayo ilimpa pesa za kulipa gharama zake katika miaka ya nyuma.

Wakati huo, Ringtone alisema, kazi  ya uchuuzi ilikuwa kazi ambayo ilimletea pesa nzuri - sio kama leo ambapo watu wanaonyeshwa kwenye mtandao na ni tofauti na miaka michache ya  hapo awali.

Akizungumzia utajiri wake, Ringtone alikiri kwamba kabla ya pesa na umaarufu sio wanawake wengi walikua wanamtaka.

Hata hivyo baada ya kupata pesa chache hapa na pale - mwimbaji huyo anasema wanawake wengi wangemkimbilia ili kupata pesa.

Hata hivyo aliwapuuza - jambo ambalo sasa anajutia kuona jinsi walivyofanikiwa tangu wakati huo na bila shaka  kusahau hali yake ya kuwa peke yake.