Juliani kununua nyumba zaidi Dandora baada ya Jengo lake kubomolewa

"Tutanunua mali nyingine hivi karibuni na sio Dandora pekee na vitongoji vyote," alisema.

Muhtasari

•Jengo hillo la Hip Hop huko Dandora lilibomolewa kutokana na kuwa karibu na mto.

•Anapanga kununua nyumba mpya huko Dandora na vitongoji vinavyozunguka ili kuendeleza misheni yake.

Juliani
Image: Facebook

Mwanamuziki Juliani amezungumza baada ya kituo chake cha Hip Hop City, Dandora, kubomolewa.

Jengo hilo ambalo lilikuwa kitovu cha kulea vipaji vya vijana katika makazi ya Dandora, lilibomolewa kufuatia agizo la serikali kutokana na kuwa karibu na mto huo.

Katika mahojiano, Juliani alieleza kuwa hakuguswa na mkasa huo, akieleza kuwa jengo hilo alipewa na Mungu na yeye ni msimamizi tu.

"Huwezi kuelewa kazi ya Mungu. Ninaendelea kuwaambia watu kwamba kila kitu ambacho nimewahi kukijenga, kwa kawaida nakiona kama sasa cha Mungu.

Mimi ni msimamizi tu anaweza kukirudisha wakati wowote. Si changu ni mali ya Mungu.

Mungu ndiye aliyenipa rasilimali za kununua jengo hilo na vitu vingine tunamwachia Mungu ndiye mtoaji.

Alipoulizwa kwa nini akupinga ubomoaji huo, Juliani alisema aikuwa na maana kufanya hivyo.

“Wenyeji walitaka kufanya maandamano na pengine kumchunguza mtu aliye nyuma ya tendo hilo.

Lakini jambo ni kwamba jengo likishaporomoka hakuna tunachoweza kufanya na sijawahi kupoteza.

 Hata mambo yanapoharibika sipotezi maana Mungu ana mpango wake,” Juliani alisema.

Alifichua mipango yake ya kununua mali nyingine huko Dandora na kitongoji chake.

 "Tutanunua mali nyingine hivi karibuni na sio Dandora pekee na vitongoji vyote," aliongeza