Hip Hop City ya Juliani katika mtaa wa Dandora yabomolewa baada ya miaka 7

Kituo hiki kimekuwepo kwa miaka saba, kikicheza jukumu muhimu katika jamii kwa kusaidia vijana kwa kukuza vipaji.

Muhtasari

•Jumba hilo  la msanii wa Kenya Juliani, Hip Hop City huko Dandora lilibomolewa Jumatatu, Mei 27.

•Ubomoaji huo ulifanywa kwa sababu ya eneo la jengo hilo kuwa karibu na mto.

Juliani
Juliani
Image: Insgaram

Mwimbaji Julius Owino, almaarufu Juliani alisikitishwa na ubomoaji wa jengo la Dandora Hip Hop City Centre katika oparesheni inayoendelea katika kaunti ya Nairobi kwa makazi yote yalio karibu na mito.

Juliani alisema anasikitika sana kwamba pamoja na jitihada zote, serikali imeendelea kubomoa kituo hicho ambacho kilikuwa mahali  vijana na wanawake walionyesha vipaji kusaidiwa kukua.

Mwimbaji huyo alishiriki video inayoonyesha tingatinga zikimbomoa kitovu jengo hilo la orofa mbili.

"Huu sio mwisho lakini inauma sana! Kufikiri kwamba tulikuwa tukifanya kazi na kupanga kupanua na kuboresha kituo hiki," Juliani alisema.

Hapo awali, alishiriki kwamba alipokea habari za ubomoaji huo unaokaribia, na aliwataka mashabiki wake wasimame naye wakati wa 'wakati wa kujaribu'.

"Tumepata habari kwamba kituo chetu cha jamii, Dandora Hip Hop City kinabomolewa. Jengo lote la ghorofa 2. Ndiyo, liko karibu na mto. Tulinunua jengo hilo zaidi ya miaka 7 iliyopita," Juliani alisema Jumapili.

Serikali imekuwa katika harakati ya kuwahamisha watu mbali na mito, haswa baada ya mafuriko ya hivi majuzi yaliyoua mamia ya watu kote nchini, wengi wao katika maeneo ya makazi duni.

Ubomoaji huo umekabiliwa na hisia tofauti kutoka kwa wakenya na viongozi. Viongozi wa upinzani wametaja ubomoaji huo kuwa wa kinyama, wakihoji ni kwa nini serikali inalenga makazi yasiyo rasmi pekee.