Shes Kemunto ataja kwa nini hayuko kwenye mahusiano

Aliangazia madhara ya kushikamana kwenye ndoa au uhusiano mbaya, akisema ndio maana bado hajafikiria kutulia na mtu yeyote.

Muhtasari

•"Acha kusubiri kitu kitokee ili uhame pengine, kufikia wakati unapoamua kuhama, pengine utakuwa umekufa," alisema.

•"Kasi ya wanawake kunyanyaswa, kuuawa na wengine kujiua kwa sababu ya masuala ya mapenzi au mahusiano inatisha,"

shes Kemunto
Image: instagram

Mwanasosholaiti wa Kenya Shes Kemunto ameeleza sababu ya kutokuwa kwenye mahusiano na mtu yeyote kwa sasa

Akizungumza kupitia kurasa zake za mitandao wa kijamii, mwanasosholaiti huyo aliangazia madhara ya kushikamana kwenye ndoa au uhusiano mbaya, na kufichua kuwa ndio maana bado hajafikiria kutulia na mtu yeyote.

Hii ni baada ya kushiriki  mazungumzo kutoka kwa watu waliokiri kudhulumiwa katika mahusiano yao ya awali.

“Mnaniuliza kama nishai pigwa kwani nafanya nini mitaa?" 

Aliendelea kuwasihi watu walio katika mahusiano kuzingatia ustawi wao na kulinda amani yao, na hiyo inakuja wakati mtu anapoona mambo yasiyo ya kawaida katika uhusiano wao na kuondoka kabla mambo kuaribika.

“Acha kusubiri kitu kitokee ili uhame pengine, kufikia wakati unapoamua kuhama, pengine utakuwa umekufa... Acha burudani hii; itakuumiza kiakili kwa muda mrefu." Aliandika Kemunto

Alitoa mfano wa watu anaowajua waliokufa na kuzikwa kwa sababu hawakuwahi kutoka katika mahusiano kwa wakati na badala yake walibaki nyuma, wakitumai mambo yangekuwa mazuri.

“Majeneza mengi sana kule chini kutokana na mahusiano mabaya una sauti nenda zako anza tena fanya kitu tu lakini usikae.”

Alimalizia kwa kuwakumbusha wanawake kutanguliza amani yao, na ikibidi kumuacha mwanaume wao atafute, iwe hivyo kwa sababu kasi ya wanawake kunyanyaswa, kuuawa na wengine kujiua kwa sababu ya masuala ya mapenzi au mahusiano. inatisha.