'Damu ya Rex haiendi hivo,' Mejja aapa kushiriki maandamano ya Jumanne kupinga mswada wa fedha

” Jana sikuweza juu ya mtoi but Tuesday 25th ni kitambi na teargas. Damu ya Rex haiendi hivo RIP ni mgenge na mbogi,” alisema.

Muhtasari
  • Kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika kwamba hakuweza kujitokeza siku ya Alhamisi kwa sababu ya majukumu ambayo hayangeweza kuepukika na mtoto wake lakini akaahidi kujitokeza Jumanne.
Mejja afichua sababu za wanaume kukwamilia wanawake warembo na wakatili.
Mejja afichua sababu za wanaume kukwamilia wanawake warembo na wakatili.
Image: Screengrab

Mwanamuziki maarufu wa Genge, Mejja alitangaza kwamba ataungana na vijana katika maandamano yajayo ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024 wenye utata.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika kwamba hakuweza kujitokeza siku ya Alhamisi kwa sababu ya majukumu ambayo hayangeweza kuepukika na mtoto wake lakini akaahidi kujitokeza Jumanne.

Alisema kuwa uwepo wake utakuwa wa kutoa heshima kwa kijana aliyedaiwa kupigwa risasi na polisi na kuaga dunia, Rex,  Alhamisi jioni alipokuwa akielekea nyumbani baada ya kupinga Mswada wa Fedha.

” Jana sikuweza juu ya mtoi but Tuesday 25th ni kitambi na teargas. Damu ya Rex haiendi hivo RIP ni mgenge na mbogi,” alisema.

Mejja ni miongoni mwa watu mashuhuri wengi wanaokataa waziwazi mswada wa fedha ambao ulilazimishwa kwa Wakenya na serikali inayotawala.

Siku ya Alhamisi, watu mashuhuri wengi wa Kenya, washawishi na waundaji maudhui waliingia barabarani kupinga Mswada wa Fedha.

Watu kadhaa mashuhuri walionekana mitaani huku waiwa wameinua mabango ya kupinga mswada wa fedha.