S2Kizzy afichua sababu ya kuwatoza wasanii Ksh 258K kurekodi nao ngoma moja

Kwa hiyo kama msanii anaweza kwenda kushoot video kwa dola 30k au 25k, dola 2k inamshinda nini?" S2Kizzy alihoji.

Muhtasari

• Hata hivyo, produsa huyo alisema kwamba kuna nyakati zingine analegeza kamba kwa wasanii chipukizi

• Ila akasisisitiza lazima chipukizi huyo "awe ba talanta kubwa SANA".

Image: Hisani

Produsa wa Tanzania, S2Kizzy amefichua kwamba ili msanii kurekodi ngoma naye, sharti atoe kiasi cha dola elfu mbili, sawa na shilingi 258k pesa za Kenya kwa wimbo mmoja.

Akizungumza na Crown Media, Produsa huyo ambaye amefanya kazi na wasanii wengi akiwemo Diamond na Alikiba alitetea kiasi hicho kikubwa akisema ndio njia pekee itakayoonyesha kuthaminiwa kwa kazi nzuri ya mtu.

"Ninaweza nikasema cha kwanza nimeshafanya sana kazi za bure. Lakini nikaja kugundua kwamba msanii anaweza kwenda kushoot video kwa dola 30k,lakini video hiyo ina dakika tatu zile zile za wimbo ule ule,"

"Kwa hiyo kama msanii anaweza kwenda kushoot video kwa dola 30k au 25k, dola 2k inamshinda nini?" S2Kizzy alihoji.

Hata hivyo, produsa huyo alisema kwamba kuna nyakati zingine analegeza kamba kwa wasanii chipukizi ila akasisisitiza lazima chipukizi huyo "awe ba talanta kubwa SANA".

"Kwa wasanii wadogo kwa mfano yule ambaye ndio anaanza kutoka huko vijijini, cha kwanza inabidi uwe na talanta kubwa sana ili kupata nafasi ya kurekodi. Cha pili lazima awe mtu fulani ambaye una adabu ili tuweze kufanya kazi," alisema.

S2Kizzy hata hivyo alidokeza kwamba msanii wa aina hiyo aghalabu hatorekodi naye bali atajipata mikononi mwa maprodusa wake ambao amewaajiri katika kampuni yake ya mapeodusa kwa jina Pluto

Lakini alisema kazi mpakq itoke mwisho kabisa lazima ipitie mikononi mwake, akisisitiza kwamba msanii kufika katika ofisi zake ghorofani, hela lazima iwepo juu ya meza kabla ya chochote kuanza.