Kutoka Kaveve Kazoze hadi Betty Kyallo: Warembo Simple Boy amekiri kuvutiwa nao kimapenzi

Stevo aliwahi nukuliwa akikiri kwamba Ngesh wa Vasha maarufu kama Kaveve Kazoze ndiye type yake na kumtaka amkubali waanze maisha ya ndoa pamoja.

Muhtasari

• “Sanaipei. Yuko konyo konyo, yaani ako milk maziwa, mtoto ako jontarira, yaani mtoto parachichi.”

wAREMBO sTEVO sIMPLE bOY ALIOWAMEZEA MATE
wAREMBO sTEVO sIMPLE bOY ALIOWAMEZEA MATE
Image: HISANI

Rapa Stevo Simple Boy kwa muda tangu aachane na Pritty Visy amekuwa askionesha uchu wake wa kimapenzi katika warembo ainati.

Kwa bahati, amekutana na baadhi ya hao anaowataka kimapenzi huku ndoto zikisalia hai kukutana na wengine ambao bado hajakutana nao.

Hii hapa ni orodha ya wanawake maarufu ambao msanii huyo wa ‘Freshi Barida’ amekuwa akiweka wazi kuvutiwa nao kimapenzi;

Kajala Masanja

Stevo wikendi iliyopita alifunguka kwa mara nyingine kwamba amekuwa akipagawa na umbo la mwigizaji mkongwe wa filamu za Bongo, Frida Kajala Masanja.

Akifungua roho yake, Stevo alisema kwamba angependa sana kuziba pengo la mahaba lililoachwa wazi zaidi ya mwaka mmoja uliopita na Harmonize katika maisha ya Kajala.

Napika chakula changu hapa. Lakini nikipika naona tu katoto fulani kanaitwa Kajala. Kajala, Kajala Kajala, mazee mi nimedata kwako, na tena umenivutia. Kajala tafadhali njoo unipikie, unioshee vyombo, unipangie nyumba,” alisema.

Betty Kyallo

Miezi 6 iliyopita, Stevo Simple Boy alionesha nia ya kuvutiwa na mtangazaji Betty Kyallo.

Akifungua moyo wake kupitia Instagram, Simple Boy aliweka wazi kwamba angefikiria kutulia kabisa katika ndopa iwapo angempata mama huyo wa binti mmoja.

“Mimi nikimpata Betty Kyalo natulia tu katika ndoa. Halafu anizalie watoto watatu, wavulana wawili na msichana mmoja. Mungu bariki maana hii yote uliumba wewe mwenyewe. Naomba sasa unibariki nayo,” Stevo aliandika huku akiichapisha picha ya Betty Kyallo.

Juhudi zake zilifua dafu siku chache baadae, baada ya kukutana kwa chakula cha jioni na Betty Kyallo.

Kamene Goro

Rapa huyo pia aliwahi nukuliwa akitema mistari yake kwa mtangazaji wa redio, Kamene Goro katika kile kilichoonekana kama ni jaribio la kutaka penzi lake.

Katika kauli zake za Julai, 2022, Stevo alifichua kwamba alikuwa amevutiwa na Goro kutokana na jinsi alivyoumbika kimahaba.

“Kamene amebeba ngongingo (amebarikiwa na mali),” mwimbaji huyo alisema. "Kamene mimi nimedata kwako, njoo kwa Stevo Simple Boy nitakupatia mapenzi simple na mambo yatakuwa welo welo,” aliongeza.

Ngesh wa Vasha

Stevo pia alionyesha kuvutiwa na mrembo kutoka kundi la wanamuziki wa Spider Clan, Ngesh wa Vasha maarufu kama Kaveve Kazoze.

Hii ni baada ya wimbo wa kundi hilo kusambaa mitandaoni na mrembo huyo kupigiwa saluti kama mmoja aliyetema mistari ya kuvutia katika wimbo huo.

Stevo alisema kwamba Ngesh ndiye alikuwa type yake haswa na kumtaka kumkubali ili waanze safari ya ndoa pamoja.

“Ngesh ni msichana mrembo, mtoto ameumbika, unaona. Lakini akuje kwangu ili tuongee tuone kama tunaweza toka kimapenzi na mambo yakiwa sawa mimi nitawaambia Wakenya ndio huyu. Pia anafaa afikirie kwamba sasa hivi kuna wanaume wengi wanamtaka lakini kuna wale pia wanakuja kudandia huo umaarufu wake, mimi nitamwambia Kaveve Kazoze ninampenda kisha wamuachilie,” Stevo alisema.

Sanaipei Tande

Julai mwaka huu, Stevo pia alikiri kwamba angependa kufanya kazi na hata kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii na muigizaji wa muda mrefu, Sanaipei Tande, akimsifia kama mrembo mwenye umbo la kipekee.

“Sanaipei. Yuko konyo konyo, yaani ako milk maziwa, mtoto ako jontarira, yaani mtoto parachichi.”