Nimekuwa heartbroken kuona Bradley amekaliwa mapajani na Pritty Vishy – Justina Syokau

“Bradley Mtall Genz Goliatha nimeumia sana kuona mtu wa ndoto zangu, mwanaume pekee nchini Kenya ambaye ana inchi ninazohitaji, mbona Pritty Vishy umekalia mtu wangu. Leo sitalala. Hii picha imeniliza.:

Muhtasari

• Hivi majuzi, kijana huyo alipokea mavazio ya viatu kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake, shukrani kwa mwanasiasa Alinur Mohamed.

• Pia, aliahidiwa ziara ya kujivinjari katika jiji la Mombasa na afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya usafirisha wa watalii, Bonfire Adventures, Simon Kabu.

SYOKAU AUMIA VISHY KUMKALIA BRADLEY
SYOKAU AUMIA VISHY KUMKALIA BRADLEY
Image: FACEBOOK

Msanii mwenye utata, Justina Syokau amekiri kuumizwa moyo na picha inayosambaa mitandaoni ya Pritty Vishy na Bradley Mtall.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Syoku alichapisha moja ya picha ya Bradley akiwa amempakata Pritty Vishy mapajani walipokutana Diani na kusema kwamba picha hiyo inamuumiza moyo.

Msanii huyo wa ‘2020’ alisema kwamba alihisi kabisa Bradley huenda akamkubali Pritty Vishy hali ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuunama penzi lake kwa mwanamume huyo anayesemekana kuwa mrefu zaidi nchini.

“Bradley Mtall Genz Goliatha nimeumia sana kuona mtu wa ndoto zangu, mwanaume pekee nchini Kenya ambaye ana inchi ninazohitaji 😭,mrefu wangu mzuri. Kusema kweli kwa nini Pritty Vishy umekalia mtu wangu. Leo sitalala. Kwanini 🤔 hukumbuki ukisaidiwa na Bishop. Hii picha inanifanya nilie,” Justina Syokau alisema.

Itakumbukwa wiki jana, Syokau alifichua kwamba Bradley Mtall ndiye mwanamume wa ndoto zake, akisema kwamba utanashati na urefu wake ndivyo vigezo amekuwa akivitafuta kwa wanaume kwa muda mrefu.

“Wakati ninasema mrefu na mtanashati, huyu ndiye ninamaanisha. Huyu kijana Bradley Mtall ndiye mwanamume wa ndoto zangu na namhitaji. Mwambieni mamtafuta sababu huwa namuota,” Syokau alisema.

“Nataka niende Dubai na wewe sababu nimeishi kukupenda Bradley Mtall, Simon Kabu ratibu haya maneno,” aliongeza.

Hivi majuzi, kijana huyo alipokea mavazio ya viatu kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake, shukrani kwa mwanasiasa Alinur Mohamed.

Pia, aliahidiwa ziara ya kujivinjari katika jiji la Mombasa na afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya usafirisha wa watalii, Bonfire Adventures, Simon Kabu.