“Unahitaji viboko” YY amjibu mtangazaji aliyelenga kujua kiini cha kuachana na mkewe

"Hata wewe unajua huwezi pata jibu, hata ukiomba ama upige misele, hakuna swali lako litajibiwa, unaharibu tu wakati. Unahitaji viboko,” YY alisisitiza.

Muhtasari

• Bila kutoa sababu kwa undani, Marya alitaka mashabiki kuheshimu faragha yao, akisema kwamba hakuwa tayari kuendelea kuzungumzia kuhusu uhusiano wake uliovunjika na YY.

YY NA MPENZIWE MARYA
YY NA MPENZIWE MARYA

Mchekeshaji YY amekula yamini kutozungumzia kuhusu ndoa yake iliyovunjika na mkewe Marya Okoth.

Aliweka hili wazi kupitia mahojiano kwa njia ya simu ya kituo kimoja cha redio humu nchini ambapo alikataa katakata kuzungumzia kilichosababisha ndoa yake kufika mwisho.

“Lakini kusema tu ukweli hata wewe si unajua ukipiga hii simu kwamba kama kuna jibu huwezi pata ni hilo. Lakini kama uko na mjazo wa simu wa kutosha na unataka kuongea wewe ongea tu lakini mimi siwezi kupa jibu. Hata wewe unajua huwezi pata jibu, hata ukiomba ama upige misele, hakuna swali lako litajibiwa, unaharibu tu wakati. Unahitaji viboko,” YY alisisitiza.

Mwishoni mwa juma lililopita, Marya Okoth kupitia Instagram alichapisha ujumbe wa kuthibitisha kwamba yeye na mumewe, YY hawangeendelea tena kuitwa mke na mume.

Bila kutoa sababu kwa undani, Marya alitaka mashabiki kuheshimu faragha yao, akisema kwamba hakuwa tayari kuendelea kuzungumzia kuhusu uhusiano wake uliovunjika na YY.

“Hamjambo na habari za asubuhi, tunasikitika kuwataarifu kwamba Marya Okoth na YY hawatokuwa pamoja tena kutokana na sababu zisizoweza kuepukika. Shukrani kwa upendo na uungwaji mkono wetu katika safari ya uhusiano wetu. Tunatumai kila mmoja wetu ataheshimu faragha yetu, ahsante,” Marya alisema kwenye waraka huo.

Katika mahojiano ya awali, Mkewe YY, Marya Okoth, alisema walianza kuishi pamoja saa moja baada ya kukutana kwa mara ya kwanza.

Akiongea na Mic Check Podcast, Marya alisema alihamia nyumbani kwa YY mara tu baada ya date yao ya kwanza. Wamekuwa pamoja tangu wakati huo na wana binti wa miaka mitatu, Circe Gaona.