Cristiano afikisha wafuasi bilioni moja mitandaoni

Ana zaidi ya wafuasi milioni 60 kwenye akaunti ya Youtube chini ya miezi miwili

Muhtasari

• Ronaldo amefikisha wafuasi bilioni moja kwenye mitandao ya kijamii mwezi mmoja baada ya kufungua akaunti ya youtube.

•Mchezaji huyu wa soka ameweka historia ya kufunga mabao mengi zaidi duniani.

RONALDO.
RONALDO.
Image: HISANI

Mchezaji nguli wa kandanda Cristiano Ronaldo amefikisha wafuasi bilioni moja katika mitandao yote ya kijamii kwa ujumla.

Cristiano ametangaza hayo kupitia mitandao yake ambapo ameshukuru jamii ya wafuasi wanaomfuatilia akisema historia imeandikwa.

"Kutoka vichochoro vya Madeira hadi majukwaa makubwa ulimwenguni, nimeishi kuchezea familia yangu na nyinyi (mashabiki), na sasa tumesimama pamoja kama bilioni moja," alisema Ronaldo.

Hivi maajuzi Ronaldo,aliandikisha rekodi ya kupata wafuasi zaidi ya milioni tano chini ya saa chache. Akaunti ya Youtube aliyofungua na kuweka video ya kwanza na mke wake Gio kufikia kuchapishwa kwa habari hii ina zaidi ya wafuasi milioni 60.6 

Aidha, Ronaldo amewashukuru wanaomfuatilia kwa uaminifu wao kwake, msaada pamoja na kuwa sehemu ya maisha yake.

"Mazuri yanazidi kuja, na tutazidi kusukuma , kushinda na kuunda historia pamoja." Aliandika Ronaldo.

Mshambuliaji huyo anazidi kuandikisha rekodi katika taaluma yake ya soka. Amefunga mabao mia tisa kitaaluma katika zaidi ya mechi 1,200 ambazo amechea timu ya taifa na vilabu.

Baadhi ya sehemu ya historia ya Cristiano Ronaldo ni kuwa mshindi wa tuzo la Ballon d'OR mara tano na mshindi nwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka UEFA mara tatu.