Hivi karibuni nitawabariki wafanyikazi wangu wa ndani kila mmoja na gari jipya – Diana Marua

Kauli ya Diana Marua kuwabariki wafanyikazi wake kwa zawadi za gari inakuja siku chache baada ya mkuza maudhui mwenzake Oga Obinna kudaiwa kumnunulia Dem wa Facebook gari jipya.

Muhtasari

• "Na hivi karibuni yaya wangu watakuwa wanaendesha magari yao. Hao ndio watakuwa wanapeleka watoto shuleni, na hilo ndilo ombi langu kwao,” aliongeza.

DIANA MARUA
DIANA MARUA
Image: INSTAGRAM

YouTuber na Rapa Diana Marua amefunguka kwamba hivi karibuni wafanyikazi wake wa ndani wataendesha magari yao mapya kama zawadi kutoka kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari za burudani wikendi iliyopita, Marua alisema kwamba ni vizuri mtu ukibarikiwa na Mungu na kujipata katika nafasi ya kuonyesha upendo kwa watu wanaokuzunguka, basi unafaa kufanya hivyo bila shruti.

“Mungu atabariki kazi ya mikono yako, mimi huwa sifanyi hivi kwa sababu ninataka malipo baadae, ninafanya hivyo kwa sababu hawa ni watu wanaonizunguka. Na nimebarikiwa kw njia Fulani, kwa hivyo mbona pia mimi nisiwabariki?” Marua aliuliza.

“Mbona nisihakikishe wanatoka kiwango kimoja kuelekea kingine? Na hivi karibuni yaya wangu watakuwa wanaendesha magari yao. Hao ndio watakuwa wanapeleka watoto shuleni, na hilo ndilo ombi langu kwao,” aliongeza.

Kauli ya Diana Marua kuwabariki wafanyikazi wake kwa zawadi za gari inakuja siku chache baada ya mkuza maudhui mwenzake Oga Obinna kudaiwa kumnunulia Dem wa Facebook gari jipya.

Obinna amekuwa akifanya kazi na Dem wa Facebook kwa miezi kadhaa sasa na amesifiwa na wengi kwa jinsi amemshika mkono mchekeshaji huyo chipukizi katika utengenezaji wa maudhui.

Miezi kadhaa iliyopita, Obinna pia alidaiwa kuwanunulia wafapiga picha wake magari kama zawadi kwa kazi nzuri wanayofanya kwenye chaneli yake ya Obinna TV.