Thee Pluto ashauri kuhusu jinsi ya kukabiliana na wenye chuki mitandaoni

Kutokana na chapisho lake anasisitiza kuwa jinsi ya kuangamiza adui si kwa uadui bali ni upendo, rehema na neema.

Muhtasari

• Youtuber Thee Pluto anapeana ushauri juu ya jinsi ya kukabiliana na wale wanaozungumza vibaya juu yako

• Anasema kuwa njia ya kuangamiza maadui ni kwa upendo, rehema na neema.

• Wiki iliyopita Pluto alitangaza kuwa wameachana na mpenzi wake Felicity Shiru, habari ambayo wengi wa mashabiki wake walisisitiza ni kiki.

THEE PLUTO
THEE PLUTO
Image: INSTAGRAM

Youtuber Thee Pluto ametoa ushauri juu ya jinsi ya kukabiliana na wale wanaozungumza vibaya katika mitandao ya kijamii.

Pluto alifunguka na kusema kuwa siku moja alifanya sherehe na kualika maadui zake wote, haswa wale ambao alijua huongea vibaya nyuma yake lakini wanadhani hajui.

Anawaonya watu kuchungana na binadamu haswa marafiki na kuwashauri wajali tabia zao wenyewe na sio sifa.

Siku moja nilifanya sherehe na kuwaalika maadui zangu wote,(Especially those I knew talk ill behind my back but think I don’t know). Days later walianza kusetiana wenyewe kwa wenyewe trying to get close to me. Ogopa binadamu. Hata kama una wafanyakazi wanaozungumza vibaya kukuhusu usipokuwepo, usiwafukuze kazi. Waangamize kwa upendo, rehema na neema. Jali tabia ako mwenyewe sio sifa,” aliandika.

Kutokana na chapisho lake anasisitiza kuwa jinsi ya kuangamiza adui si kwa uadui bali ni upendo, rehema na neema.

Hivi majuzi, Pluto alitangaza kuachana na mpenzi wake Felicity Shiru, habari ambayo mashabiki wake wengi walikataa kuamini na kusema kuwa ni kiki.

Youtuber huyo alitumia instastory yake kusisitiza kuwa habari hiyo ni ya ukweli.

“Hakuna kitu chochote cha kufanyia mzaha kuhusu taarifa niliyotoa awali, ni kweli kuna muziki unakuja lakini hilo ni suala lingine kivyake na tulishafanya video tayari. Kuhusu kuachana, sifanyi mzaha, ni kweli tumeshaachana,” Pluto aliandika.

Japo kuwa wana video ya wimbo ambayo walishiriki pamoja na ambayo itatoka hivi karibuni, Pluto alisema kwamba hilo halina chochote kuhusiana na kuachana kwao.