“Hii vita inahitaji amani na ubunifu tu!” Alikiba kuhusu Crown TV kushindana na Wasafi TV

“Hivyo ukitaka kulenga kwenye mapambano utapigana peke yako. Vita yenyewe inahitaji Amani tu na ubunifu kidogo. Tunafanya yetu tu na wao wafanye yao,” aliongeza.

Muhtasari

• “Hivyo ukitaka kulenga kwenye mapambano utapigana peke yako. Vita yenyewe inahitaji Amani tu na ubunifu kidogo. Tunafanya yetu tu na wao wafanye yao,” aliongeza.

ALIKIBA NA DIAMOND
ALIKIBA NA DIAMOND
Image: HISANI

Afisa mkuu mtendaji wa lebo ya muziki ya Kings Music na shirika la habari la Crown Media, Alikiba amezungumzia kuhusu lengo kuu la kuanzisha chombo cha habari licha ya kujua kwamba kuna vituo vingi tu vya habari tayari.

Akizungumza kuelekea uzinduzi wa runinga ya Crown TV,ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuzindua kituo cha redio – Crown FM, Alikiba alisema kwamba lengo si kushindana na vituo vingine vya runinga.

Alikuwa anamjibu mwandishi wa habari aliyetaka kujua ni jinsi gani Crown TV itakuja na upekee kuhakikisha wameshindana na ikiwezekana kuwapiku washindani wao ambao tayari wamo kabisa kwenye kazi.

Hata hivyo, Alikiba alibainisha kwamba lengo si kupambana na vituo vingine kama Wasafi TV ambacho kinatajwa kuwa ndicho mlengwa mkuu wa ushindani kutokana na ujio wa Crown TV.

Alisema kwamba wao kama Crown TV watahakikisha wanafanya upande wao na kuwapa mashabiki kilichobora na wala si kujikita katika kushindana na wenzao kwa mfanano wa vipindi na matangazo.

“Lengo sio mapambano, lengo ni kuwapa watu kilicho bora zaidi kwa sababu hapa ni nyumbani. Wacha wao wafanye vizuri kwa sababu ndiyo ndoto ya kila mtu na ndivyo inavyotakiwa kufanya vizuri. Wao wafanya yao na sisi tufanye yetu,” alisema.

“Hivyo ukitaka kulenga kwenye mapambano utapigana peke yako. Vita yenyewe inahitaji Amani tu na ubunifu kidogo. Tunafanya yetu tu na wao wafanye yao,” aliongeza.

Msanii huy mapema mwaka huu alitangaza ujio wa shirka lake la habari – Crown Media ambalo litajumuisha kituo cha redio na runinga.

Miezi kadhaa baadae, alizindua stesheni ya redio ambayo ilianza kupeperusha vipindi vyake hawani na kumaliza ngoja ngoja ya zaidi ya miezi miwili tangu kutoa tangazo rasmi.

Hata hivyo, mashabiki wamekuwa wakihji kuhusu ujio wa kituo cha runinga na kuona vipindi vyake, hoja ambazo Alikiba amejibu kwamba tayari wamo katika hatua za lala salama kuanza kuenda hewani moja kwa moja.