Produsa S2Kizzy amuomba Zuchu kumuunganisha na mama yake, Khadija Kopa

Aligundua kwamba anaweza kupata fursa nzuri ya kumfikia Kopa kwa kupitia mwanawe ambaye sasa ni msanii tajika katika lebo hiyo kubwa nchini Tanznania, Zuchu.

Muhtasari

• “Nimekuwa nikitamani kufanya kazi na malkia Khadija Kopa, tafadhali Zuchu fanya mpango basi,” aliandika.

KHADIJA KOPA
KHADIJA KOPA
Image: INSTA

Mtayarishaji wa muziki kwa wasanii wengi kutoka Bongo, S2Kizzy amemuomba msanii wa WCB Wasafi, Zuchu kumuunganisha na mama yake, mkali wa Taarab Khadija Kopa.

Kupitia instastory yake, S2Kizzy alifichua kwamba kwa muda mrefu amekuwa akitamani kufanya kazi na malkia wa mipasho, Khadija Kopa lakini kwa bahati mbaya hajawahi fanikiwa kumfikia.

Aligundua kwamba anaweza kupata fursa nzuri ya kumfikia Kopa kwa kupitia mwanawe ambaye sasa ni msanii tajika katika lebo hiyo kubwa nchini Tanznania, Zuchu.

Alimuomba kufanya mpango ili kufanikisha ndoto zake zimetimia.

“Nimekuwa nikitamani kufanya kazi na malkia Khadija Kopa, tafadhali Zuchu fanya mpango basi,” aliandika.

Kupitia instastory yake, Zuchu alichukua taarifa hiy na kumjibu S2Kizzy akisema kwamba maadamu lishafika kwake, ajue kwamba limekwishapitishwa tayari.

“Ushanipa kesi, haya limeisha,’ Zuchu alimjibu S2Kizzi.

S2Kizzy amejizolea umaarufu katika siku za hivi karibuni kwa kuwa mfyatuaji wa madunde ambayo yanafanya vizuri kwa wasanii kutoka mirengo yote.

Ndiye produsa wa pekee ambaye amefanikiwa kuwauzia wasanii kutoka Konde gang ya Harmonize, Kings Music ya Alikiba na WCB Wasafi ya Diamond na ngoma zao zote zikafanya vizuri na kushindania nafasi kwenye chati za muziki.

S2Kizzy amekuwa tajika kwa kuleta mtindo mpya wa midundo ya Amapiano ya Kibongo ambay imekuwa ikifanywa na wasanii wengi.

Kwa upande mwingine, Khadija Kopa ni maarufu kwa miziki yake ya rusharoho na mipasho ya taarab tangia miaka ya awali akifanya pia kolabo ya wasanii kama vile Diamond na bintiye mwenyewe, Zuchu.