Zari afunguka kuhusu uhusiano wa Zuchu na watoto wake, ammiminia sifa kemkem

Alisema kuwa kamwe hana uhusiano mbaya na wanawake wa Diamond.

Muhtasari

•Zari ameweka wazi kuwa yeye huwa sawa  kila mara watoto wake wanapomtembelea baba yao Diamond Platnumz nchini Tanzania.

•Zari alimmwagia sifa kemkem mpenziwe Diamond akifichua kuwa hata watoto wake Tiffah Dangote na Prince Nillan wanampenda.

Zari, Diamond na wapenzi wao
Zari, Diamond na wapenzi wao
Image: Instagram

Mwanasosholaiti mashuhuri kutoka Uganda Zari Hassan ameweka wazi kuwa yeye huwa sawa  kila mara watoto wake wanapomtembelea baba yao Diamond Platnumz nchini Tanzania.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari wa Tanzania siku ya Alhamisi, mama huyo wa watoto watano alisema kwamba huwa hana shida na watoto wake kuwa chini ya uangalizi wa baba yao na mpenzi wake Zuhura Othman almaarufu Zuchu.

Alisema kuwa kamwe hana uhusiano mbaya na wanawake wa Diamond.

“Watu wanachukulia eti mimi siongei na wanawake wa Diamond, naongea na Mama J, naongea na Zuchu,” Zari alisema.

Aliongeza, “Ata kama watoto wanakuja Tanzania, simtafuti ata Baba T kumwambia nini kinaendelea, mko poa? Nampigia, namwambia za asubuhi, what’s happening? Alafu ananiambia.

Mwanasholaiti huyo mwenye umri wa miaka 43 alimmwagia sifa kemkem mpenziwe Diamond akifichua kuwa hata watoto wake Tiffah Dangote na Prince Nillan wanampenda.

“Sioni tatizo. Kwanza yeye ni msichana mzuri sana, yeye ni msichana mzuri sana, na watoto wangu wakiwa huku, they are very comfortable kuwa naye . Mara nyingi huwa wanasema,” alisema.

Haya yanajiri wiki kadhaa tu baada ya mwanasosholaiti kushtumiwa kwa kuvunja mahusiano ya Zuchu na Diamond Platnumz.

Shida ilidaiwa kuanza baada ya video iliyomuonyesha Zari Hassan akitembea huku akiwa ameshikana mikono na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Bosi huyo wa WCB alikuwa wa kwanza kuchapisha video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alimtambulisha mama huyo wa watoto wake wawili kama dada yake.

“Mimi na dada @zarithebosslady,” Diamond aliandika chini ya video hiyo.

Video hiyo iliyosambazwa mwezi Februari ilizua hisia mseto kutoka kwa wanamtandao tofauti ambao walitaka kuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Zari hata hivyo alikanusha madai ya kuvunja uhusiano wa Diamond na Zuchu akisema, "Kwani promotion ya nyimbo inaingiliaje kwa mapenzi, kwani kaka ashoot na wanawake wengine, nitolee upuuzi."