Zari azua wasiwasi baada ya kuchapisha ujumbe wa kimafumbo kuhusu mahusiano

Alisema kuwa mara tu uongo unapoibuka, mtu ambaye alidanganywa anakosa utulivu kabisa.

Muhtasari
  • Ujumbe wake unajiri siku chache baada ya mpenziwe Shakib Cham kufafanua kuwa alikuwa na mchumba hapo awali

Mwanasosholaiti na mjasiriamali kutoka Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini Zari Hassan aamewaacha mashabiki wake na maswali mengi yasiyo na majibu baada ya kupakia ujumbe mzito kwenye akaunti yake ya snapchat.

Ujumbe wake unajiri siku chache baada ya mpenziwe Shakib Cham kufafanua kuwa alikuwa na mchumba hapo awali.

Kupitia snapchat, mama huyo wa watoto watano alishiriki nukuu ya Horacio Jones kuhusu jinsi uwongo unavyoathiri uhusiano.

"Baadhi ya watu hawaelewi jinsi uongo ulivyo na sumu. Uongo huambukiza na kulaani uhusiano wenye furaha hadi unahisi kuumwa na tumbo lako kwa kuwaamini tena," Zari aliandika.

Mfanyabiashara huyo aliongeza kuwa mara tu uongo unapoibuka, mtu ambaye alidanganywa anakosa utulivu kabisa kwani hawawezi kuwa na uhakika wa kile wanachoambiwa.

"Hata kama unampenda mtu kiasi gani, wakati mwingine huwezi kujizuia kujisikia kama ameiba Faraja yako. Huna raha tena kwa sababu unabahatisha kila kitu. Sasa, kuwaamini sio kazi ngumu. Sasa inahitaji mtu bidii na wakati mwingine hiyo inachosha." Zari aliongeza.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na kituo kimoja cha televisheni nchini Uganda, Shakib alinukuliwa akithibitisha kwamba alichumbiana na Mimi ambaye anaishi U.S.A miaka minane iliyopita lakini hakuwahi kumuoa.

“Namfahamu Shakirah Nalule, na alikuwa mpenzi wangu miaka minane iliyopita lakini sikuwahi kumuoa

"Alitamani hata niende Marekani nikiwa Afrika Kusini, lakini nilikataa baada ya kugundua kuwa sisi sote tunatoka ukoo mmoja, "Ngonge" sio tu kwamba pia ana watoto sita kutoka kwa wanaume tofauti," Shakib alielezea.