CECAFA: Ko'galo yawatwanga Maniema Union

Gor Mahia ilicharaza Maniema Union ya DRC Congo 2-1 kwenye mchuano wao wa kwanza kwenye kundi D kwenye michuano ya Kagame Cup inayoendelea kule Rwanda. Gor Mahia imo kwenye kundi moja na Ports FC, KMKM  ya Uganda na Maniema ya DRC congo.

Kwenye michuano hio ambapo wachezaji Tobias Otieno na Dickson Ambundo  walipata nafasi za kuichezea Gor Mahioa mechi zao za kwanza baada ya kukamilisha usajili wao kutoka Sony. kocha Hassan Oktay amesema kuwa alifurahishwa na jinsi sajili zake zinavyoonyesha ukomavu wao.

Kwenye mechi za kundi A, green Eagle ililaza Heegan magoli mawili bila jibu huku APR FC ya Rwanda ikicharaza Proline 1-0. Kundi B, KMC FC ilitoka sare ya goli kwa moja na Atlabara FC ya Sudan Kusini huku Bandari Fc kutoka Kenya ikitoka sare hiohio na Kampala City ya Uganda.

Bingwa mtetezi wa taji hili, Azam yumo kwenye kundi C pamoja na Mukura, TP Mazembe ya Congo na Rayon Sports ya Rwanda. Kwenye mechi ya kwanza Azam ililaza Mukura goli moja bila jibu huku Rayon Sports  ikilaza TP Mazembe goli moja bila jibu.