Champions League: Mabingwa Liverpool wakalifishwa na Napoli

napoli
napoli
Liverpool walipoteza 2-0 kwa Napoli katika nechi yao ya ufunguzi ya ligi ya mabingwa awamu ya makundi huku mabao mawili ya Dries Mertens na Fernando Llorente yakiwapa waItalia ushindi.

Wakati huo huo kocha wa Chelsea Frank Lampard alipoteza mechi yake ya kwanza ya kipute hicho 1-0 kwa Valencia ugani Stamford Bridge. Barcelona nao walitoka sare tasa na Borussia Dortmund, huku nahodha Lionell Messi akichukua mahala pa Ansu Fati mwenye umri wa miaka 16 katika mechi yake ya kwanza.

Inter Milan nao pia walitoka sare ya 1-1 na Slavia Prague, huku Ajax wakiwalaza Lille mabao 3-0.

Shida za mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City ziliendelea baada ya mlinzi John Stones kupata jeraha la msuli litakalomweka nje kwa muda wa mwezi mmoja au zaidi.

Haya yanajiri wiki mbili pekee baada ya mlinzi mwenzake Aymeric Laporte kupata jeraha la goti litakalomweka nje hadi Februari mwaka ujao.

City sasa wamesalia na Nicolas Otamendi kama mlinzi wa kati pekee mwenye tajriba kubwa. Kiungo wa Brazil Luiz Fernandinho atachukua mahala pa Stones.

Hayo yakijiri, shirikisho la riadha nchini limempa fursa mwanaridha Kumari Taki kuchukua mahala pa bingwa wa dunia Eijah Manang'oi katika kikosi cha mita 1,500 kitakachoshiriki mbio za ubingwa duniani jijini Doha, Qatar mwezi huu.

Haya yanajiri baada ya Manang'oi kutangaza kuwa atakosa kutetea taji lake kutokana na jeraha la kisigino. Taki alimaliza wanne katika mbio za mchujo, lakini atajiunga na nduguye Manangoi George Manangoi, Timothy Cheruiyot na Ronald Kwemoi katika kikosi cha Kenya kitakachokua kikiwania dhahabu.