Chile kuchuana na Columbia katika robo finali ya Copa America

Baada ya michuano ya makundi kufanyika wiki mbili zilizopita, sasa mataifa manne yamefuzu katika awamu ya robo fainali.

Mwenyeji Brazil aliyeongoza kundi A anatarajiwa kuchuana na taifa la Paraguay mnamo tarehe 28 mwezi huu katika uwanja wa Arena Do Gremio.

Argentina yake Lionel messi inatarajiwa kuchuana na taifa la Venezuela mnamo tarehe 28 saa 10:00 usiku.

Ratiba ya robo fainali za copa America

  1. Brazil vs Paraguay
  2. Argentina vs Venezuela
  3. Chile vs Colombia
  4. Uruguay vs Peru

Mshindi wa mechi ya kwanza atakutana na mshindi wa mechi ya pili huku mshindi wa mechi ya tatu akikutana na mshindi wa mechi ya nne. Fainali ya Copa America itachezwa mnamo tarehe saba mwezi julai mwaka 2019.

Kwingineko ni kuwa taifa la Mexico limekamilisha orodha ya mataifa yaliyo fuzu kwenye awamu ya robo fainali ya Goldcup CONCACAF.

Mataifa mengi yaliyo fuzu kwenye robo fainali hizo ni pamoja na :Haiti, Canada, Costa Rica,Jamaica, panama, U.S.A pamoja na Curacao.

Ratiba ya mechi za Robo finali za Concacaf

  1. Haiti vs Canada
  2. Mexico vs Costa Rica
  3. Jamaica vs Panama
  4. U.S.A vs Curacao