Covid 19: 14 zaidi wafariki huku visa vipya 788 vya coronavirus vikiripotiwa

Kenya leo imesajili visa vipya 788 vya coronavirus huku  jumla ya idadi ya visa hivyo  ikifikia   9,913.

Visa hivyo vipya  vimetokana na sampuli  5,521  ambazo zilipimwa katika kipindi cha  saa 24 zilizopita .

Kati ya visa hivyo 788 ,785 ni wakenya ilhali 3 ni vya raia a kigeni . katibu wa uwala wa afya Rashid Aman amesema wagonjwa 100 wamepona  na kufikisha jumla ya watu

8,121 ambao wamepona ugonjwa huo nchini .hata hivyo watu 14 wameaga dunia na kufikisha 325 jumla ya walioaga dunia kutokana na ugonjwa huo