David Beckham afichua kuwa analenga kumsajili Mbappe kama mteja wake

mbappe
mbappe
Mchezaji wa zamani wa Uingereza na nahodha David Beckham anamlenga mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kama mteja wake wa kwanza katika kazi yake mpya kama ajenti . (Mail)

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Man United Mark Robins amesema kwamba ilikuwa rahisi kwake kukataa kuwa mkufunzi wa Sunderland na kuamua kutia saini kandarasi mpya na klabu ya Coventry. (talksport)

Ajenti mmoja raia wa Urusi anadai kwamba aliiomba klabu ya Zenit St - Petersburg kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexander Lacazette ambaye alikuwa anagharimu £61m . (mirror)

Kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba ,26, anakaribia kupona jeraha tayari kucheza mechi dhidi ya Liverpool mnamo tarehe 20 mwezi Oktoba licha ya ripoti ya kuvunjika kidole. (sun)

Man United inaweza kutarajia ufadhili wa shati utaokagharimu £450m huku wakisaka kandarasi mpya. (ESPN)

Aston Villa imehusishwa na kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25. (Birmingham Mail)

Kazi ya Unai Emery kama mkufunzi Arsenal huenda ipo hatarani iwapo kikosi chake kitashindwa kufuzu katika kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu . (Times - subscription required)

-BBC