David 'Calabar' Owino amejumuishwa katika kikosi, asema Bobby Williamson

Picha: sirlotan.wordpress.com

Kocha wa Harambee Stars Bobby Williamson amesema David Owino anayecheza soka yake huko Zambia amejumuishwa katika kikosi cha stars kinachojitayarisha kuchuana na Cape Verde mwezi ujao.

Owino kwa jina la utani 'Calabar' hakuwa katika kikosi cha awali cha Harambe Stars. Kwingineko mchezaji wa Gor Mahia Inncoent wafula ametemwa kutoka kikosi cha Harambe Stars kitakachochuana na cape verde na katika mechi za kombe la Cecafa.