Arda Güler: Kinda wa Real Madrid afichua kwa nini hawaiti Modric na Kroos kwa majina yao

Arda Güler Alisema kuwa huwa hawaita kwa majina yao akisema kuwa alifunzwa katika familia yake kuita mtu aliyekuzidi umri kwa jina lake ni ishara ya kumkosea heshima.

Muhtasari

• Kadhalika, alitaja kuwa wanamwita “Abi” jambo ambalo anaona linamvutia kwa sababu hawajui maana yake katika lugha ya Kituruki ambayo itakuwa “kaka”.

ARDA GULER.
ARDA GULER.
Image: FACEBOOK

Arda Güler, kinda wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 19 amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na wachezaji wakongwe wa klabu hiyo, Luka Modric na Toni Kroos.

Akizungumza na jarida la nchini kwao Uturuki, Sportskafa, Arda Güler alifichua majina ambayo yeye huwaita wakongwe hao wenye umri wa miaka 38 na 34 mtawalia.

Arda Güler Alisema kuwa huwa hawaita kwa majina yao akisema kuwa alifunzwa katika familia yake kuita mtu aliyekuzidi umri kwa jina lake ni ishara ya kumkosea heshima.

“Siwezi kuwaita Kroos au Modric kwa majina yao, nahisi hiyo ni kuwadharau. Namwita Toni kaka na Luka pia, kwa hivyo walianza kuniita kaka pia," alisema mchezaji huyo mchanga wa Real Madrid.

Kadhalika, alitaja kuwa wanamwita “Abi” jambo ambalo anaona linamvutia kwa sababu hawajui maana yake katika lugha ya Kituruki ambayo itakuwa “kaka”.

Hatimaye, alizungumza kuhusu kwa nini aliamua kusaini Madrid na kuondoka Fenerbahce katika umri mdogo.

"Ningeweza kusalia Fenerbahçe kwa mwaka mwingine, lakini nilitaka kuonyesha ulimwengu kile mchezaji mdogo wa Kituruki angeweza kufanya Ulaya. Natumai kuendelea kuthibitisha."

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 aliandika jina lake katika kumbukumbu za historia ya Los Blancos kwa kuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo kufunga katika mechi yake ya kwanza ya La Liga katika klabu hiyo.

Bao lake kuu dhidi ya Real Sociedad mnamo Ijumaa, Aprili 26, lilipata ushindi muhimu wa bila bila, na hivyo kuimarisha nafasi ya Madrid kileleni mwa La Liga.