DCI yakita kambi kwa afisi za Nick Mwendwa kutokana na matumizi mabaya ya pesa

Maafisa kutoka afisi za ujasusi nchini DCI wamemhoji kiongozi wa shirikisho la Soka nchini Nick Mwendwa kuhusiana na matumizi mabaya ya pesa. Kulingana na taarifa, milioni 244 zilitolewa na serikali wakati wa michezo ya dimba la Afrika na ambazo Mwendwa ameshindwa kuelezea namna zilivyotumika.

Inadaiwa kuwa Mwendwa alifika katika afisi za DCI na baadhi ya wafanyakazi katika ofisi zake ili kujibu madai ya ufujaji wa pesa baada ya wizara ya michezo kulalamikia hatua ya matumizi mabaya ya pesa ambazo ilikuwa imepatia FKF.

Serikali inataka ufafanuzi zaidi wa kuhusiana na jinsi pesa hizo zilivyotumika .

Katibu wa zamani wa michezo Peter Kaberia ambaye kwa sasa yuko katika wizara ya Madini alikuwa miongoni mwa watu waliofikishwa mbele ya DCI.

Kwa sasa, taarifa zinasema kuwa Mwendwa alishindwa kujibu maswalia aliyokuwa anaulizwa na sasa faili ya kesi yake itafikishwa kwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma DPP.

Hatamu ya Mwendwa ilitamatika Febrauri 10 mwaka huu japo ameshikilia kuwa yungali kiongozi wa michezo nchini hadi pale kiongozi mwingine atakapochaguliwa..