Dybala ataka malipo ya pauni 350,000 kama atajiunga na Man United

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, mwenye umri wa miaka 25, anataka malipo ya pauni 350,000 kwa wiki ikiwa atajiunga na Manchester United. (Sun)

Kiungo wa kati wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes, anayehusishwa na taarifa za kuhamia Tottenham na Manchester United, ameliambia gazeti la Sporting Lisbon kuwa anataka kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu . Sporting wanaamini atataka euro milioni 70 au pauni £64m kwa ajili ya nahodha huyo mwenye umri wa miaka 24 . (Record, via Mirror)

Manchester United wanasemekana kusaini mkataba na Fernandes baada ya kombe la Super Cup la Portugal . (Express)

Tottenham wanataka mchezaji mbadala wa kukaba nafasi iwapo watamuuza Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, baafda ya muda wa mwisho wa kipindi cha kuhama kwa wachezajii cha waingereza kukamilika Alhamisi. Klabu za Uhispania zina hadi Agosti 31 kusaini mkataba na wachezaji . Pamoja na Fernandes, Spurs wanafanya mazungumzo na Real Betis kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Argentina Giovani lo Celso, mwenye umri wa miaka 23. (London Evening Standard)

Arsenal wanatarajia kutoa ofa mpya kwa ajili ya kiungo wa kati- wa Celtic Kieran Tierney katika siku zijazo , baada ya kukataliwa dau mbili za awali kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uskochi mwenye umri wa miaka 22 . (Sky Sports)

kiungo wa kati wa Chelsea na wa timu ya kimataifa ya Ufaransa N'Golo Kante, mwenye umri w amiaka 28, anasisitiza kuwa atakuwa Stamford Bridge msimu huu, licha ya taarifa zinazomuhusisha na Paris St-Germain. (Express).

Dau la Manchester City kwa ajili ya mchezaji wa safu ya ulinzi ya Juventus na Ureno Joao Cancelo, mwenye umri wa miaka 25, atakuwa Danilo na kuondoka klabu hiyo . Akiwa na umri wa miaka 28 mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil anaweza kujiunga na Wataliano. (Manchester Evening News)