Everton wako tayari kuipa changamoto Arsenal kumuwania Wilfried Zaha

zaha
zaha

Leo ikiwa Jumapili tarehe 21, mwezi Julai mwaka wa 2019 zifuatazo ni tetesi za soka bara ulaya.

Everton wako tayari kuipa changamoto Arsenal kumuwania mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, ambaye anauzwa na klabu yake ya Crystal Palace kwa kitita cha pauni milioni 80. (Evening Standard)

Manchester United, Everton na Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Juventus kuhusu kumsajili Blaise Matuidi. (Le Parisien).

Manchester United wanaongeza jitihadi kumpata kiungo wa Lazio, mzaliwa wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic. (Mirror)

Inter Milan wanamtaka mchezaji wa Man United Lukaku.

Livepool inamtaka beki wa kushoto wa Augsburg Philipp Max, 25, (Sport)

Tottenham na West Ham wanamtolea macho Diego Llorente, 25 wa Real Sociedad. (El Mundo Deportivo)

Wolverhampton Wanderers wanataka kumsajili mshambuliaji wa Italia na AC Milan Patrick Cutrone mwenye thamani ya takriban pauni milioni 20. (Express & Star)

Tottenham imempa mkataba mpya wa mwaka mmoja mshambuliaji Fernando Llorente. (Mail)

Crystal Palace imetangaza dau la pauni la milioni 8 kumpata kiungo wa Everton James McCarthy. (Sky Sports)

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amemaliza matumaini ya Everton kwa kumsajili Kurt Zouma ambaye aliutumia msimu uliopita akiwa Goodison Park kwa mkopo. (Mirror)

Mshambulizi Edin Dzeko, 33, huenda akaondoka Roma baada ya miaka mitatu, huku Inter Milan ikiwa na mpango wa kupata saini ya mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 15.(Sportitalia)

-BBC