Gabu amsifia msanii Diamond Platnumz

gabu.bugubugu
gabu.bugubugu
Msanii mkubwa Afrika mashariki Gabu almaarufu kama Bugubugu alipata nafasi na kufika kwenye kikao cha Papa Na Mastaa kinachoruka kupitia mtandao wa youtube wa Redio Jambo.

Kikao hiki huongozwa na mtangazaji Rais Papa  na huwa ni kitengo maridhawa cha mazungumzo na mastaa wakubwa nchini.

Gabu ameweza kuzungumzia nyimbo yake na msanii Mbosso kutoka lebo ya WCB huku akimsifia msanii nguli Afrika na mmiliki wa Wasafi FM na Wasafi TV Diamond Platnumz.

"He's a good businessman. Very sharp. Anajua chenye anafanya."

Soma habari kemkem:

Staa Gabu ameweza kuzungumzia nyimbo inayotamba kwa sasa Koroga na sababu kubwa za kuichapisha katika mtandao wa Vevo.

"Vevo inalipa vizuri. Vevo ni ya mastaa. Na pia watu wengi wanatoka Youtube na kwenda kwa Vevo. Halafu ina rangi nzuri katika TV yako nyumbani. Nimependa tu vevo."

Katika nyimbo hii inayofanya vizuri katika mtandao huo, Gabu alifunguka jinsi walivyoshirikiana na staa kutoka Uganda Addy Andre na Arrowboy.

Soma hadithi hapa:

"Niliita Arrowboy akakuja kwa studio nikampatia collabo nikamwita Addy andre kutoka Uganda ni producer na bado mi msanii amefanyia Jose Chameleone kwa hivyo akakuja Kenya tukafanya muziki. Tukasafiri Tanzania tukafanya video na Kenny kwa siku 3.  Kenny anafanya na Zoom Production Wasafi alafu video ikatoka."

Mkali huyu wa Koroga pia alizungumzia kuhusu collabo yake na Mbosso kutoka lebo ya WCB, Mastory huku akionekana kubana kiwango cha hela alichomlipa.

Soma mengine hapa:

“Mambo ya hela sitataja. Chenye nitakwambia ni tuliclick vizuri mambo yakawa sawa ile siku alikuwa amekuja Nairobi. Tukaclick vizuri alikuja kwa studio yangu Kompakt Records tukarekodia audio hapo alafu tukaenda Tanzania kushoot video. Tuko na uhusiano kati ya Kompakt na Wasafi."

Hali kadhalika Gabu alimzungumzia msanii Kristoff na jinsi anavyomwona kisanii

"Kristoff tumetoana mbali nimeweza kum_advise hapa na pale. Na Kristoff sasa ni one of the biggest artistes hapa Kenya. Sisi ni marafiki tu, family friends na business men.

Soma hapa:

Msanii huyu alieleza kimya cha kundi la Punit ambayo wengi wamekuwa wakihisi kuwa kuna ubaridi ambao ni dalili ya kuvunjika kwa kikundi hiki.

"Timu tupo lakini tuko na bigger fish to fry. Mimi niko na studio yangu hapo nmeshikana na Steve Ongechi. Boneye na studio yake pale Decimal Records ameshikana na Musyoka. Frasha alikuwa ndani ya Pacho. Idea yetu ni kushikilia industry in various ways but tunakuja pamoja tunafanya kama Punit na kila mtu ni brand kivyake."

Gabu amesema kuwa yupo na mpango imara wa kuhakikisha kuwa anawasaidia wasanii chipukizi kupitia studio yake

"Kwa studio kuna wasanii tunawabring up hapo Kompakt Records  in the few months hivi mtakuwa mnawaskia. Kuna nyimbo ya kimataifa nafuatilia ila chenye nafuatilia sai ni my new artiste anatoa ngoma".

Soma hapa: