Amerika kuisadia Kenya kukabiliana na ufisadi

Picha kwa hisani ya: independent.co.uk

Marekani itaisadia Kenya kupambana na ufisadi, kurejesha mali iliyoibwa nchini na kuzuia kuhamishwa kwa fedha zilizofujwa na maafisa wa umma.

Katika makubaliano ya hoja 29 yaliotiwa saini kati ya Kenya na marekani wakati wa ziara ya rais Barack Obama, Kenya imeahidi kuzidisha juhudi za kupambana na ulaji rushwa ikiwemo kuwataja maafisa wakuu wa serikali wanaohusishwa na sakata za ufisadi.

Mkuu wa sheria Githu Muigai amesema serikali itatekeleza makubaliano hayo.