IEBC kutoa adabu kali ya kisheria dhidi ya KANU

Picha: The Star

IEBC imetishia kukichukulia hatua za kisheria chama cha KANU baada ya viongozi wake Gideon Moi, ambaye pia ni Seneta wa Baringo ya Kati, na Nick Salat kususia mkutano na tume hiyo.

Afisa mtendaji wa tume hiyo, Ezra Chiloba, amesema tume hiyo huenda ikazuia chama hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao, akihoji kuwa chama hicho hakikuwasilisha ushahidi wowote dhidi ya madai yake, ya kwamba IEBC ilitumia teknolojia kuiba kura katika uchaguzi mdogo uliofanyika County ya Kericho wiki jana, ambapo mgombea kiti wa chama cha Jubilee Aaron Cheruiyot alichaguliwa kuwa Seneta mpya wa eneo hilo.